MAHAKAMA KUTOA UAMUZI KWENYE KESI YA MVUVI NAKURU

Maafisa 6 wa idara ya wanyamapori nchini KWS wanaohusishwa na kutoweka kwa mvuvi Brian Odhiambo mwanzoni mwa mwaka jana katika mbuga ya wanyama ya Lake Nakuru watafahamu iwapo wana kesi ya kujibu au la tarehe 3 mwezi ujao. Kulingana na hakimu mkuu wa mahakama ya Nakuru Kipkurui Kibelion, mahakama itazingatia ushahidi uliotolewa na upande wa […]

SERIKALI INACHUNGUZA ‘MGENI’ ALIYEWAHADAA WANAWAKE

Hofu imeibuka kuhusiana na usalama wa wanawake nchini kutokana na ripoti ya raia mmoja wa kigeni kudaiwa kuwahadaa wanawake kadhaa na kuwapeleka katika makazi yake nchini, akarekodi na kusambaza picha za siri za wanawake hao bila idhini yao wala ufahamu wa idara ya ujasusi. Kulingana na msemaji wa serikali Isaac Mwaura, idara ya usalama, upelelezi […]

LEBRON HAJUI MUSTAKABALI WAKE NBA

Nyota wa mpira wa kikapu wa LeBron James amesema hana uhakika kama ataendelea kucheza zaidi ya msimu huu, ambao ni wa 23 kwake katika ligi ya mpira wa kikapu ya Marekani. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 41, anayekipiga katika klabu ya Los Angeles Lakers, alizungumza kabla ya mchezo wa nyota bora wa ligi hiyo, […]

AMBANI ALALAMIKIA UKOSEFU WA MABAO

Kocha wa AFC Leopards, Fred Ambani, amelalamikia ukosefu wa umakini wa kutikisa nyavu baada ya timu yake kutoka sare ya bila mabao dhidi ya Bandari katika Uwanja wa Mbaraki, jana. Licha ya sare hiyo, Ambani aliwasifu wachezaji wake kwa kuonyesha moyo wa kupambana chini ya hali ya hewa ya ukanda wa pwani aliyoitaja kuwa ngumu na […]

AKONNOR ASIFU GOR MAHIA

Kocha wa Gor Mahia, Charles Akonnor, ameisifu timu yake kwa nidhamu ya uchezaji baada ya ushindi mgumu wa mabao 2–1 dhidi ya APS Bomet katika Uwanja wa Kericho Green, Jumapili. Ushindi huo umeihakikishia Gor Mahia pointi tatu muhimu na kupanua uongozi wake kileleni mwa FKF Premier League hadi tofauti ya pointi sita. Akonnor amesema timu iliingia uwanjani kwa tahadhari […]

LIZ ANDIEGO AINGIA NGUMI ZA KULIPWA

Bondia wa kike mwenye mafanikio makubwa nchini, Liz Andiego, sasa amejiunga rasmi na ngumi za kulipwa, akifungua ukurasa mpya katika taaluma yake. Bondia huyo mwenye umri wa miaka 37 atapanda ulingoni kwa mara ya kwanza kama mtaalamu Februari 27, 2026, jijini Nairobi, ambapo atamenyana na Chiku Iddi wa Tanzania katika pambano la raundi nne uzani […]

WAMALWA AZUNGUMZIA VIFO KITENGELA

Kiongozi wa Chama cha DAP Kenya, Eugene Wamalwa, amesema watu wawili walifariki na takribani Wakenya 50 kujeruhiwa wakati wa mkutano wa Linda Mwananchi uliofanyika Kitengela. Akizungumza katika mkutano na wanahabari Wamalwa ameeleza masikitiko yake na kudai kuwa kulikuwa na matumizi ya nguvu kupita kiasi. Aidha, ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuingilia kati akisema kuna ongezeko la […]

OTIENDE AONYA KUHUSU MGAWANYIKO NDANI YA ODM

Mbunge wa Rarieda, Otiende Amollo, ameonya kuhusu kuongezeka kwa mgawanyiko ndani ya chama cha Orange Democratic Movement, akisema mvutano huo unaweza kuathiri mazungumzo ya kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2027. Akizungumza katika eneo bunge lake, Otiende amesisitiza kuwa anaendelea kuwa mwaminifu kwa chama hicho, lakini akakiri kuwa kimegawanyika katika makundi yanayopingana. Aidha, Otiende ameonya kuwa migawanyiko hiyo […]

MARAGA AUNGA MKONO MALALAMISHI YA UPINZANI

Kiongozi wa chama cha UGM, David Maraga, amesema anaunga mkono malalamishi ya upinzani kuhusu matumizi ya vitoa machozi na maafisa wa polisi katika mikutano ya kisiasa. Akizungumza katika Kaunti ya Meru, Maraga amesema kuna haja ya kuchukuliwa hatua dhidi ya maafisa wanaodaiwa kuzua vurugu na kutumia nguvu kupita kiasi. Aidha, ameungana na wito wa upinzani […]

KUPPET BUNGOMA YALALAMIKIA SHA

Viongozi wa muungano wa kutetea maslahi ya walimu wa shule za upili na vyuo vya kadri KUPPET tawi la Bungoma North wameitaka serikali kuchukua hatua za haraka ili kutatua ugumu wanaopitia kupata huduma za matibabu chini ya bima ya SHA. Kulingana na viongozi hao, walimu wamekuwa wakisafiri mwendo mrefu ili kupata vituo vya afya vinavyowahudumia […]