WAKILI WILLIS OTIENO ATOA USHAURI KUHUSU UPIGAJI KURA

Wakili wa jiji Willis Otieno amewahimiza Wakenya kupiga kura kwa kutumia kumbukumbu badala ya hisia, huku juhudi za uhamasishaji wa kiraia zikiendelea kushika kasi nchini. Kupitia taarifa kwenye akaunti yake ya X Otieno ameeleza kuwa kupiga kura kwa kutumia kumbukumbu kunamaanisha kuimarisha uwajibikaji kwa viongozi katika ngazi ya wananchi. Aidha, wakili huyo amesisitiza umuhimu wa […]

KALUMA ASEMA ODM ITAWAACHILIA BAADHI YA VIONGOZI

Mbunge wa Homa Bay mjini Peter Kaluma amesema chama cha ODM kitawaachilia rasmi baadhi ya viongozi wake wakuu wakati wa Mkutano wa Taifa wa Wawakilishi (NDC) unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni. Kaluma amesema hatua hiyo itawalenga Gavana wa Siaya James Orengo, Mbunge wa Embakasi East Babu Owino, Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna na Seneta wa Vihiga Godfrey Osotsi. […]

KAMATI YA BUNGE YAIDHINISHA FEDHA KULIPA MADENI YA NHIF

Kamati ya Bunge ya Afya imeidhinisha ombi la Wizara ya Afya la kutenga shilingi milioni 5.3 kusaidia kulipa madeni ya Mfuko wa Bima ya Afya wa Taifa (NHIF) yanayodaiwa na vituo mbalimbali vya afya. Hatua hiyo inalenga kupunguza mzigo mkubwa wa madeni unaoathiri vituo vya afya vinavyodai serikali, hali inayochangia kudorora kwa utoaji wa huduma […]

PVK YAKOSOA SIASA ZA MATUSI MIONGONI MWA VIONGOZI

Muungano wa Pentecostal Voice of Kenya ukiongozwa na Mwenyekiti wake ambaye pia ni Kiongozi wa Kanisa la Jesus Teaching Ministry Apostle Peter Manyuru umekosoa kuongezeka kwa utamaduni wa matusi na uhasama wa kisiasa miongoni mwa viongozi, ukionya kuwa hali hiyo inachochea mgawanyiko na kudhalilisha hadhi ya uongozi wa umma. Katika taarifa kwa vyombo vya habari, muungano huo […]

NOTTINGHAM, VILLA NA PALACE ROBO FAINALI ULAYA

Klabu ya Aston Villa itamenyana na Bologna katika robo fainali ya mashindano ya UROPA, baada ya kuandikisha ushindi wa jumla ya mabao 3-0 dhidi ya Lille ya Ufaransa jana usiku. Mabao ya John McGin na Leon Bailey jana usiku yaliihakikishia ushindi Villa yake Unai Emery, na kuwapa nafasi katika awamu hiyo wanapolenga kurejea katika mashindano […]

FIFA YAPITISHA SHERIA MUHIMU KWA SOKA YA WANAWAKE

Timu zote zinazoshiriki mashindano ya soka ya wanawake zitahitajika kuwa na makocha au makocha wasaidizi wanawake. Hii ni baada ya shirikisho la soka ulimwenguni, FIFA, kupitisha sheria hiyo hapo jana katika mkutano wa baraza lake. Sheria hiyo itaanza kutekelezwa katika mashindano ya kombe la dunia kwa wanawake wasiozidi umri wa miaka 20 mwezi Septemba, na […]

KIVUMBI CHATARAJIWA KATI YA GOR VS SHABANA FC

Kinyang’anyiro kikali kinatarakiwa wikendi hii katika ligi ya soka, KPL, viongozi Gor Mahia watakapovaana na Shabana FC hapo kesho ugani Nyayo. K’Ogalo wataingia katika mtanage huo wakiwa uongozini kwa pointi 53 baada ya mechi 24, Shabana nao wakiingia uwanjani wakiwa na shinikizo baada ya kichapo mara 2 mfululizo, matokeo ambayo yamesababisha kufutwa kwa kocha wake […]

3 WAZUILIWA MUMIAS KWA TUHUMA ZA UNAJISI

Polisi katika kituo cha polisi cha Shianda eneo bunge la Mumias East wanatarajiwa kuwafikisha mahakamani wanaume 3 akiwemo mhudumu wa boda boda wanaoshukiwa kuwanajisi wasichana wenye umri wa miaka 10 kwenye matukio mawili tofauti. Akithibitisha kukamatwa huko, kamanda wa polisi eneo hilo Dorice Chemoss amesema mwathiriwa wa kwanza kutoka eneo la Dorofu alikuwa akielekea Shianda […]

WALIOANGAMIA KWENYE AJALI KISII KUZIKWA LEO

Watu 6 waliouawa kupitia ajali ya barabara katika eno la Kegati kwenye barabara ya Kisii-Keroka wiki mbili zilizopita watazikwa hii leo katika hafla tofauti kwenye eneo bunge la Nyaribari Chache. 6 hao waliangamia baada ya trela lililoripotiwa kukata breki, kupoteza mwelekeo na kuwagonga katika soko la Kegati. Ibada ya pamoja ya mazishi kwa 6 hao […]

BOMOA BOMOA NAIROBI KUDHIBITI MAFURIKO

Serikali ya kaunti ya Nairobi imeanzisha zoezi la kuyabomoa majumba yote yaliyo kwenye njia za mito, zoezi ambalo limeanzia katika eneo la Westgate katika juhudi za kudhibiti athari za mafuriko. Ubomozi huo unatekelezwa kwa mujibu wa mapendekezo ya kamati ya mpito ya jiji ambayo imesema majumba yote yaliyo kwenye njia za mito yataathirika. Gavana wa […]