VIJANA WACHUKUA MWELEKEO MPYA WA UCHAGUZI

Vijana nchini wameonyesha ari ya kuhakikisha sauti zao zinasikika kwenye uchaguzi mkuu ujao, kutokana na idadi yao kubwa ambayo sasa imeanza kujitokeza kusajiliwa kama wapiga kura, wakiapa kuwachagua viongozi walio tayari kuwajibika. Katika siku za hivi karibuni, maelfu ya vijana wamejitokeza kusajiliwa na kusababisha changamoto kwa upande wa IEBC kushughulikia idadi ya juu, vijana hao […]

GACHAGUA AIBUA MADAI DHIDI YA RUTO

Aliyekuwa naibu Rais Rigathi Gachagua ameibua madai kwamba Rais William Ruto amezizuia kampuni zote za Uchina dhidi ya kutekeleza miradi humu nchini, na kwamba rais ameiruhusu kampuni 1 pekee. Akizungumza jijini Nairobi, Gachagua amedai kuwa rais ana uhusiano wa karibu na kampuni hiyo ambayo huenda inatumiwa kufuja fedha za umma. Imetayarishwa na Antony Nyongesa

VIJANA WATARAJIA AJIRA ZA SGR

Mamia ya vijana nchini wanatarajiwa kunufaika na nafasi za ajira kwenye mradi wa ujenzi wa awamu ya pili ya reli ya kisasa, SGR, kutoka Naivasha kuelekea Malaba kupitia Kisumu ambao umeratibiwa kukamilishwa ndani ya miaka 2. Akizungumza baada ya kuzindua mradi huo wa shilingi bilioni 500, Rais William Ruto amesema kuwa reli hiyo itarahisisha usafirishaji […]

CARRICK AMTAKA TUCHEL KUWAPA NAFASI WACHEZAJI WA MAN UNITED

Kocha wa muda Manchester United Michael Carrick amemtaka kocha wa timu ya taifa ya England Thomas Tuchel kuwapa nafasi wachezaji wa klabu hiyo kuthibitisha uwezo wao kuelekea Kombe la Dunia. Carrick amewataja Harry Maguire, Luke Shaw na Kobbie Mainoo kama wachezaji wanaostahili kupewa nafasi, akibainisha kuwa hawajateuliwa tangu Tuchel achukue usukani wa timu hiyo Januari […]

ARSENAL YAPATA MOTISHA KABLA YA FAINALI DHIDI YA MAN CITY

Mshambuliaji wa Arsenal Leandro Trossard amesema ushindi wao kwenye UEFA Champions League dhidi ya Bayer Leverkusen ni maandalizi bora kuelekea fainali ya Kombe la Ligi dhidi ya Manchester City. Arsenal walifuzu kwa hatua ya robo fainali baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Leverkusen, na kufanikisha ushindi wa jumla wa mabao 3-1, huku City wakiondolewa […]

METTE AFUNGUA USHINDANI KIKOSINI TUSKER FC

Kocha mkuu wa Tusker Julien Mette amesema hakuna mchezaji aliyehakikishiwa nafasi ya kuanza kikosini, akisisitiza kuwa uteuzi utafanywa kwa kuzingatia uwezo na juhudi za kila mmoja. Kocha huyo raia wa Ufaransa amesema msimamo huo tayari umechochea ushindani mzuri katika nafasi mbalimbali, hasa langoni ambapo ushindani umeongezeka kwa kiasi kikubwa. Kipa mpya Pavelh Ndzila alivutia katika […]

KABRAS SUGAR WABADILI MKAKATI LICHA YA KUONGOZA LIGI

Mabingwa watetezi Kabras Sugar wamelazimika kubadili mkakati wao msimu huu licha ya kumaliza juu ya jedwali la Kenya Cup, kocha mkuu Carlos Katywa amesema. Akizungumza baada ya kukamilika kwa hatua ya ligi kuelekea nusu fainali, Katywa amesema msimu huu umekuwa na changamoto tofauti ikilinganishwa na misimu iliyopita ambapo walitwaa ubingwa. Klabu hiyo inalenga kushinda taji […]

CHEBOI ASUSIA MWALIKO WA SENETI

Gavana wa Kaunti ya Baringo County Benjamin Cheboi amesema hatahudhuria vikao vya Seneti kufuatia mvutano unaoendelea kati ya taasisi hiyo na magavana. Cheboi alieleza kuwa hatohudhuria mikutano hiyo hadi pale Seneti itakaposhughulikia kwanza mgogoro uliopo kati yake na viongozi wa kaunti. Aidha, gavana huyo ameitaka Seneti kutatua tofauti zake na magavana kabla ya kuwaita viongozi […]

MTU MMOJA AFARIKI BAADA YA MAFURIKO TRANS NZOIA

Mvua kubwa inayoendelea kunyesha katika Kaunti ya Trans Nzoia imesababisha majonzi na uharibifu mkubwa baada ya mtu mmoja kupoteza maisha kwa kusombwa na mafuriko. Kwa mujibu wa ripoti kutoka eneo la Namajalala, mto Sabwani ulivunja kingo zake na kusababisha maji kutiririka kwa kasi kuelekea katika maeneo ya makazi. Tukio hilo limesababisha hofu miongoni mwa wakazi […]

MAHAKAMA YA JUU YATETEA UHALALI WA MFUKO WA BIMA YA AFYA

Mahakama Kuu imeidhinisha uhalali wa Mfuko wa Bima ya Afya ya Jamii (SHIF) huku ikibaini kuwa utekelezaji wake kitaifa haukuzingatia viwango vya kikatiba kutokana na mapungufu ya kiutaratibu na kiutendaji. Katika uamuzi wake, Jaji Bahati Mwamuye amesema kuwa ingawa mfumo wa kisheria unaouongoza mfuko huo ni thabiti, namna ulivyotekelezwa ilikiuka haki muhimu za kikatiba ikiwemo haki ya utu […]