HOSPITALI YA NAIROBI YAJITETEA KUHUSU HALI YA KIFEDHA

Hospitali ya Nairobi imetetea hali yake ya kifedha na uendeshaji wake ikisema huduma zinaendelea bila kukatizwa, huku ikilaumu mgogoro wa muda mrefu wa uongozi kwa taharuki iliyoshuhudiwa mahakamani na hadharani. Katika mkutano na wanahabari, mwenyekiti wa bodi Barcley Onyambu pamoja na Afisa Mkuu Mtendaji Felix Osano wamesema hospitali hiyo iko imara na inaendelea kutoa huduma kikamilifu […]

RUTO AZINDUA UJENZI WA RELI YA KISASA YA SGR

Rais William Ruto amezindua rasmi ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR kutoka Naivasha kuelekea Kisumu na Malaba, baada ya kuweka jiwe la msingi katika viwanja vya Chuo cha Ualimu cha Narok. Mradi huo wa urefu wa kilomita 475 unatarajiwa kupita katika maeneo ya Naivasha, Narok, Bomet, Kericho, Nyamira, Kisumu hadi mpaka wa Malaba. Akizungumza […]

KLABU ZA UINGEREZA ZADHALILISHWA UEFA

Timu ya Newcastle United ya Uingereza ilikalifishwa kwa kichapo cha mabao 7-2 na Barcelona ya Uhispania, na hivyo kubanduliwa nje ya mashindano ya klabu bingwa bara Ulaya. Barcelona walitinga robo fainali kwa jumla ya mabao 8-3 kufuatia sare ya bao 1-1 katika mechi ya mkondo wa kwanza, na watacheza na wenzao wa La Liga Atletico […]

UJIO WA AUMA WATARAJIWA KUIMARISHA LIONESSES

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya wanawake ya raga Kenya Lionesses Simon Odongo, ameonyesha Imani ya kuimarika kwa kikosi chake kutokana na kurejea kwa Judith Auma, timu hiyo inapojiandaa kwa mkondo wa pili HSBC SVNS Div 2 jijini Montevideo, Uruguay wikendi hii. Half-back huyo wa Impala RFC anarejea kutoka mkekani kutokana na jeraha la […]

BAO LA SSENYONJO LAWAPA INGWE USHINDI

AFC Leopards walifufua matumaini ya kuwania ubingwa wa taji la ligi kuu ya soka, KPL, kufutia ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Nairobi United ugani Nyayo hapo jana. Wakiwa na machungu ya kufungwa mabao 4-1 na Mathare United, Ingwe walirejea uwanjani humo kuwapa matumaini mashabiki na usimamizi wa klabu hiyo. Bao ya majaribio na […]

UTABIRI: MVUA KUONGEZEKA IJUMAA

Mvua inayoendelea kwa sasa katika maeneo mbali mbali ya nchi inatarajiwa kuongezeka na kufikia mililita 20 kati ya leo na Jumanne wiki ijayo, wananchi wakionywa kuhusu uwezekano wa mafuriko ya ghafla. Katika utabiri wake, idara ya utabiri wa hali ya anga imesema maeneo yatakayoathirika ni pamoja na kaunti za Turkana, West Pokot, Samburu, Migori, Bungoma, […]

WAFANYAKAZI WA VIWANJA VYA NDEGE KUGOMA TENA

Mamlaka ya viwanja vya ndege nchini ina muda wa siku 6 kushughulikia malalamishi ya wafanyakazi wa viwanja hivyo ambao wameonya kuwa watagoma na kutatiza shughuli katika viwanja hivyo iwapo ilani yao itapuuzwa. Kwenye makataa ya siku 7 yaliyotolewa hapo jana, muungano wa wafanyakazi hao, KAWU, unataka mamlaka hiyo itekeleze makubaliano yaliyotiwa saini mwezi jana, mbali […]

VYUO VIKUU VYAMEZWA NA MADENI

Wizara ya elimu imelitaka bunge kuidhinisha bajeti ya ziada ya shilingi bilioni 14.3 ili kuvinusuru vyuo vikuu vya umma nchini vinavyokabiliwa na hatari ya kufungwa kutokana na madeni ya zaidi ya shilingi bilioni 100. Akiwa mbele ya kamati ya bunge kuhusu elimu, katibu mkuu katika idara ya elimu ya juu Dakta Beatrice Inyangala, amesema kuna […]

NYUFA ZAIDI ODM MIKUTANO SAMBAMBA IKIANDALIWA

Tofauti za kisiasa zimejitokeza zaidi ndani ya chama cha ODM baada ya makundi hasimu chamani humo ambayo ni Linda ground lake kinara Oburu Oginga na Linda Mwananchi la katibu mkuu Edwin Sifuna, kutangaza kuandaa mikutano sambamba ya kitaifa ya wajumbe mwezi huu. Mrengo wa Sifuna umetangaza kwamba mkutano wao uliopewa jina la People’s National Delegates […]

WAWILI WAKWAMA JENGONI WESTLANDS

Shughuli za uokoaji zinaendelea katika eneo la Westlands jijini Nairobi kuwakoa wafanyakazi wawili waliokwama baada ya sehemu ya jengo la ghorofa 22 kuporomoka usiku wa kuamkia leo. Kwa mujibu wa shirika la msaada la Kenya Red Cross, wafanyakazi wawili waliokolewa bila majereha, na kuongeza kuwa hali ya waliokwama bado haijulikani. Mkasa huo unajiri siku 2 […]