STARS WAJIANDAA KUNG’AA KWENYE MASHINDANO YA FIFA

Timu ya taifa ya wanaume ya soka Harambee Stars inatarajiwa kuondoka leo nchini kuelekea Rwanda baada ya kufanya mazoezi yao ya mwisho hapo jana ugani Nyayo jijini Nairobi. Stars watashiriki mechi za kirafiki katika mashindano ya 2026 FIFA Series, ambayo yamezinduliwa kwa lengo ya kuyawezesha mataifa fursa za kushiriki mechi za kimataifa. Kocha mkuu Benni […]

ZAIDI YA 66 WAAGA KWENYE AJALI COLOMBIA

Watu wasiopungua 66 wameripotiwa kuaga dunia baada ya ndege ya kijeshi iliyokuwa imewabeba watu 125 kuanguka ilipokuwa ikijaribu kupaa nchini Colombia. Kulingana na maafisa wa serikali, ndege hiyo iliyokuwa na maafisa wa kijeshi 114 na wafanyakazi 11 wa ndege, ilianguka katika eneo la Leguizamo, mpakani pa taifa hilo la Ecuador na Peru. Waziri wa ulinzi […]

ODM: TUTAMPA RUTO MGOMBEA MWENZA

Wadhifa wa atakayekuwa mgombea mwenza wa Rais William Ruto kwenye uchaguzi mkuu ujao umeendelea kuibua gumzo, viongozi wa chama cha ODM kutoka Pwani wakitaka wadhifa huo kutengewa ODM. Kauli za viongozi hao zinajiri huku wenzao wa UDA kutoka Mlima Kenya wakishikilia kuwa wadhifa huo utasalia mikononi mwa naibu rais wa sasa Kithure Kindiki. Hata hivyo, […]

GEN Z WAHIMIZWA KUJIANDIKISHA KUPIGA KURA

Vijana wa kizazi cha Gen Z nchini wamehimizwa kujitokeza kwa wingi na kusajiliwa kama wapiga kura ili kuafikia mageuzi ya uongozi wanayoshinikiza kupitia uchaguzi mkuu wa mwaka ujao. Akizungumza katika kaunti ya Kiambu, aliyekuwa naibu Rais Rigathi Gachagua, amesema hatua hiyo itawawezesha kuwatimua kutoka uongozini viongozi wanaoendeleza dhuluma dhidi ya vijana hao. Alikuwa ameandamana na […]

WANASIASA WAONYWA DHIDI YA UTEKAJI NYARA

Idara ya usalama nchini imewaonya viongozi wa kisiasa dhidi ya kuibua madai ya kutekwa nyara kwa lengo la kutaka kuhurumiwa na wapiga kura, ikisema wahusika watakabiliwa kulingana na sheria. Onyo hii imetolewa baada ya Waziri wa zamani Raphael Tuju kujitokeza kutoka mafichoni, mkurugenzi wa idara ya upelelezi wa jinai DCI, Mohammed Amin akikariri kwamba Tuju […]

HARVEY BARNES KUCHUKUA NAFASI YA EZE KATIKA TIMU YA UINGEREZA

Mchezaji wa Newcastle, Harvey Barnes, anatarajiwa kuitwa katika kikosi cha England chini ya Thomas Tuchel kuchukua nafasi ya Eberechi Eze aliyejeruhiwa. Eze hakuwemo katika kikosi cha Arsenal katika fainali ya Carabao Cup Jumapili ambapo walipoteza 2-0 dhidi ya Manchester City kutokana na jeraha la mguu wa chini. Barnes tayari amewahi kuitwa mara moja mnamoOktoba 2020, ikiwa ni […]

BB BREAD FC KUKABILIANA NA KENYA POLICE KWENYE FKF CUP

Klabu ya BB Bread  italazimika kucheza kwa kiwango cha juu ikiwa wanataka kufuzu hatua ya robo fainali ya FKF kwa mara ya tatu mfululizo, baada ya kuteuliwa kukabiliana na Kenya Police katika raundi ya 16, kulingana na droo iliyofanywa kwenye Uwanja wa Taifa wa Nyayo. Bread FC tayari wameiondoa AFC Leopards na Gor Mahia kufikia […]

SERIKALI KUJIKWAMUA ILI KUFANIKISHA AFCON 2027

Serikali imeonyesha kujiamini katika kukidhi vigezo vya shirikisho la  Soka Barani Afrika (CAF) kabla ya mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka 2027, yatakayoandaliwa na Kenya, Uganda, na Tanzania. Katibu Mkuu wa Michezo, Elijah Mwangi, ameekiri kwamba nchi bado haijatekeleza wajibu wake mkuu, uliokuwa ni malipo ya ada ya kuwa mwenyeji. Kenya inatakiwa kukusanya dola milioni […]

WAATHIRIWA WA MAFURIKO TRANS NZOIA WATAKA KUHAMISHWA

Waathiriwa wa mafuriko katika eneo la Namanjalala, kaunti ya Trans Nzoia, wanataka kuhamishiwa katika maeneo salama kufuatia athari kubwa za mafuriko. Wakazi hao wanasema maisha yao yako hatarini huku wakikosa makazi ya kudumu baada ya mafuriko kuharibu makazi yao. Mafuriko hayo yalisomba nyumba pamoja na mali zao, na kuwaacha wengi bila makazi wala mahitaji ya […]

MAFURIKO YAWASUMBUA WAKAZI ELDORET

Mamia ya wakazi wa jiji la Eldoret wameshindwa kutoka majumbani mwao kufuatia mafuriko yaliyoshuhudiwa katika maeneo mbalimbali. Mto Sosiani umefurika na kuelekeza maji katika maeneo ya makazi, hali iliyosababisha uharibifu na kuhatarisha maisha ya wakazi. Maeneo yaliyoathiriwa zaidi ni pamoja na mtaa wa Elgon View ambako wakazi wanakabiliana na athari za mafuriko hayo. Imetayarishwa na […]