KINDIKI AJIBU GACHAGUA KUHUSU UHALIFU WA MERU

Naibu Rais Kithure Kindiki amejibu kauli za mtangulizi wake Rigathi Gachagua kufuatia onyo la siku kumi alilotoa kuhusu kukomesha uhalifu wa kutumia silaha katika eneo la Meru Kaskazini, kaunti ya Meru. Kauli hiyo ya Kindiki inajiri baada ya Gachagua kutishia kuhamasisha wakazi wa maeneo yanayokumbwa na mashambulizi hayo kujihami iwapo serikali haitachukua hatua ndani ya muda uliowekwa. Kindiki amemtupia […]

KOOME AONYA TUME YA ARDHI KUHUSU UADILIFU

Jaji Mkuu Martha Koome ameitaka Tume ya Kitaifa ya Ardhi kuzingatia uadilifu na uwazi katika utekelezaji wa majukumu yake. Akizungumza wakati wa kuapishwa kwa makamishna wapya wa tume hiyo, Koome amesisitiza umuhimu wa uwajibikaji ili kujenga imani ya wananchi. Wakati huo huo, makamishna wapya wa tume ya ardhi nchini wameapishwa rasmi kuanza kuhudumu katika majukumu […]

EACC YAONYA WANASIASA DHIDI YA MATUMIZI MABAYA YA MALI YA UMMA

Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi nchini (EACC)  imetoa onyo kwa wanasiasa walio madarakani dhidi ya kutumia mali ya umma kuendesha kampeni zao. Wakizungumza jijini Nakuru , viongozi wa tume hiyo wamesisitiza umuhimu wa uadilifu katika utumizi wa rasilimali za umma. Aidha, wameeleza kuwa ufisadi umeorodheshwa kama janga la pili nchini baada ya tatizo la ukosefu […]

DCI YACHUNGUZA KUTOWEKA KWA TUJU 

Idara ya upelelezi wa jinai DCI, imesema inaendeleza uchunguzi kuhusiana na taarifa za kutoweka kwa Waziri wa zamani Raphael Tuju, ambaye hajulikani aliko tangu Jumamosi. Kulingana na familia iliyopiga ripoti ya kutoweka kwake hapo jana, Tuju alitoweka na dereva wake, walipokuwa njiani kuelekea kwa shirika moja la habari kwa mahojiano, gari lake likiripotiwa kupatikana katika […]

POLISI WACHUNGUZA ‘MAPENZI YA ASIDI’ NAIROBI

Polisi mtaani Kibra jijini Nairobi wameimarisha uchunguzi katika tukio ambapo mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 24 anauguza majeraha hospitalini baada ya kuripotiwa kumwagiwa asidi na mshukiwa anayeaminika kuwa mpenziwe. Mary Clare, aliyekuwa kitoka kazini, alishambuliwa kwenye barabara ya Ngong akiwa na rafiki yake, katika kinachoamini kuwa kuwa mzozo wa kimapenzi. Tayari mshukiwa mmoja anazuiliwa […]

SHILINGI LA KENYA YADUMISHA THAMANI

Shilingi ya Kenya imesalia dhabiti dhidi ya sarafu kuu mwishoni mwa wiki jana, ikisaidiwa na mahitaji makubwa ya wawekezaji wa dhamana za serikali, kulingana na ripoti ya wiki ya Benki Kuu ya Kenya, CBK. Bei ya ndani imefungwa kwa Ksh129.52 kwa kila dola ya Marekani Machi 19, ikilinganishwa na Ksh129.30 Machi 12, ikionyesha kushuka kwa […]

UHABA WA MAFUTA WARIPOTIWA NCHINI

Uhaba wa mafuta umeanza kushuhudiwa katika maeneo mbalimbali nchini huku madereva wakiripoti kuyakosa vituoni, licha ya serikali kusisitiza akiba ya kitaifa bado iko thabiti. Katika jiji la Nairobi, baadhi ya vituo vya mafuta vimeripotiwa kukosa kabisa petroli na dizeli na kuanza kuuza kwa vipimo, na madereva wengi wamelazimika kuzunguka kutoka kituo kimoja hadi kingine wakitafuta […]

CARABAO: CITY WAZIMA NDOTO YA MATAJI 4 KWA ARSENAL

Manchester City walizima matumaini ya Arsenal kushinda mataji 4 msimu huu, baada ya kuwapa kichapo cha mabao 2-0 ugani Wembley kunyakua ubingwa wa dimba la Carabao kwa mara ya 9. Nico O’Reilly alifunga mara 2 na kumhakikisha mkufunzi Pep Guardiola ubingwa mara 5 wa kombe hilo, na kumfanya kuwa kocha wa kwanza kushinda kombe la […]

UBINGWA WA CAF: BERKANE, SUNDOWNS WATINGA NUSU FAINALI

Klabu za RS Berkane ya Morocco na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini zilitinga awamu ya nusu fainali ya mashindano ya klabu bingwa barani Afrika katika mechi za mkondo wa pili wa robo fainali zilizokamilika hapo jana. RS Berkane walihitaji muda wa ziada kufunga bao la ushindi, Mounir Chouiar akifuta makosa yake ya awali ya kupoteza […]

LEOPARDS WAMWAGA MVINYO WA TUSKER FC

Klabu ya AFC Leopards iliimarisha uwindaji wake wa ubingwa wa ligi kuu ya soka nchini, KPL, msimu huu, baada ya kuandikisha ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Tusker FC. Baada ya kipindi kirefu cha tahadhari kwa timu zote 2 katika uwanja wa Nyayo, Leopards walitoa kucha zao na kuumwaya mvinyo, kupitia kwa Hassan Beja […]