STAGE 3 YA SAFARI RALLY YAFUTILIWA MBALI

Siku ya pili ya mashindano ya Safari Rally imetatizika mapema baada ya hatua ya 3 yaani Stage 3, SS3 Camp Moran ya mashindano hayo kufutiliwa mbali rasmi kutokana na hali mbaya ya barabara. Kwa mujibu wa waraka karani wa mashindano hayo George Mwangi, uamuzi huo umechukuliwa kwa misingi ya usalama kufuatia kuharibika kwa barabara kutokana […]

TIMU ZA WANAWAKE FKF-WPL ZASUSIA MECHI

Huenda ratiba ya mechi za ligi ya wanawake nchini, FKF-WPL, ikasambaratika baada ya klabu zinazoshiriki ligi hiyo kutangaza kuwa hazitacheza mechi zozote za ligi kuanzia wikendi hii hadi shirikisho la soka nchini, FKF, litakaposhughulikia malalamishi yao. Kupitia waraka uliotiwa saini na klabu 11 kati ya 12 za ligi hiyo, timu hizo zimetaka kikao na Rais […]

HOFU YA ONGEZEKO LA GHARAMA MBAGATHI

Wabunge wameibua hofu kuhusu kuongezeka kwa gharama ya ujenzi wa hospitali ya rufaa ya huduma ya kitaifa ya polisi ya Mbagathi, ambayo sasa imefikia shilingi milioni 833, kutoka makadirio ya awali ya shilingi milioni 400. Wakizungumza wakati wa kikao na Inspekta mkuu wa polisi Douglas Kanja, wanachama wa kamati ya bunge kuhusu usalama wametaja hatua […]

NAIROBI, VIUNGA VYAKE KUPATA MVUA

Mvua ya kiwango cha kati hadi kubwa inatarajiwa jijini Nairobi na viunga vyake katika kipindi cha saa 24 zijazo. Katika taarifa yake iliyotolewa hapo jana kuhusu hali ya anga, idara ya utabiri wa hali ya anga imesema mvua hiyo itaathiri maeneo ya nyanda za juu zilizo mashariki mwa bonde la ufa ikiwemo Nairobi kufikia leo […]

NPS YATAKA MABILIONI ZA UCHAGUZI

Huku washikadau mbali mbali wakijiandaa kwa uchaguzi mkuu wa mwaka ujao, idara ya polisi imelitaka bunge kuitengea mgao wa shilingi bilioni 21 zaidi ili kufanikisha maandalizi yake, ikiwemo ununuzi wa magari kwa baadhi ya vituo vya polisi. Akiwa mbele ya kamati ya bunge kuhusu usalama, Inspekta Mkuu wa polisi Douglas Kanja, amesema kuwa idara hiyo […]

MGAO WA ELIMU KUONGEZEWA KSHS 65B, RUTO

Sekta ya elimu nchini inataratajiwa kuboreshwa katika kipindi cha mwaka mmoja ujao kutokana na mpango wa serikali kuongeza mgao wa sekta hiyo kwa shilingi bilioni 65 kwenye mwaka wa kifedha wa 2026-27. Kulingana na Rais William Ruto, nyongeza hiyo ni sehemu ya mpango wa kuboresha sekta ya elimu, akisema serikali yake inaendelea kufanikisha utekelezaji wa […]

MECHI ZA EUROPA: ASTON VILLA WASAKA USHINDI

Michuano ya Ligi ya Europa itaandaliwa usiku wa Leo huku timu kadhaa zikipania kujiweka sawa katika mkondo wa kwanza wa mechi hizo. Saa tatu kasorobo itashuhudia mechi kadhaa ikiwemo Stutgart dhidi ya Porto, Bologna wavaane na Roma, huku Lille ya Ufaransa wakipambana na Aston Villa. Saa tano itashuhudia Nottingham Forest wakicheza dhidi ya Midjylland, Genk […]

NYABERI BADO ANA MATUMAINI YA KUPANDA DARAJA

Kocha wa Fortune Sacco FC, Vincent Nyaberi, amesema timu yake bado ina nafasi nzuri ya kupanda daraja kutoka Ligi ya National Super League licha ya kushika nafasi ya sita kwenye msimamo wa jedwali. Nyaberi amesema bado wana matumaini ya kumaliza miongoni mwa timu tatu bora ifikapo mwisho wa msimu. Matumaini hayo yaliimarika Jumamosi baada ya […]

BUYACHI: NIDHAMU ITASAIDIA OILERS KUISHINDA KABRAS

Kocha msaidizi wa Menengai Oilers, Lawi Buyachi, amesema utulivu na nidhamu vitakuwa muhimu timu yake itakapokutana na mabingwa Kabras Sugar RFC katika mechi ya Ligi ya Kenya Cup itakayochezwa Jumamosi katika uwanja wa Kakamega Showground. Timu ya Oilers kutoka Nakuru bado haijafanikiwa kuishinda Kabras katika mikutano 14 tangu ipandishwe daraja hadi ligi kuu katika msimu […]

MAHAKAMA YATUPILIA MBALI KESI INAYOPINGA UTEUZI WA NOORDIN HAJI

Mahakama Kuu imetupilia mbali ombi lililokuwa likipinga kuteuliwa kwa Noordin Haji kama Mkurugenzi wa Huduma ya Kitaifa ya Ujasusi (NIS) iKisema kuwa uamuzi wa Rais katika kuwateua maafisa wakuu wa umma ni wa hiari yake na unalindwa na Katiba. Katika uamuzi wake, mahakama iMEbainisha kuwa hoja za waliowasilisha kesi hiyo kwamba Haji hakupaswa kuteuliwa kutokana na […]