EACC YAWAHIMIZA WAKENYA KUKUMBATIA MFUMO WA FAINI ZA PAPO HAPO

Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC) imewataka Wakenya kuunga mkono mfumo wa Mamlaka ya Kitaifa ya Usafiri na Usalama Barabarani (NTSA) wa kutoza faini za papo hapo kwa madereva wanaokiuka sheria za trafiki. Hata hivyo, wito huo unatolewa licha ya Mahakama kusitisha kwa muda utekelezaji wa mfumo huo kufuatia changamoto za kisheria zilizoibuliwa […]

WANAFUNZI 11 WAANGUKA NDANI YA SHIMO LA CHOO KAPSABET

Mwanafunzi mmoja amefariki na Wengine 10 wa Shule ya wasio na uwezo wa kusikia ya Kapsabet wamelazwa hospitalini baada ya kuanguka ndani ya shimo la choo lililoporomoka katika eneo la shule hiyo hilo wakati wanafunzi hao walipokuwa wakikimbilia kushuhudia msafara wa Rais William Ruto uliokuwa ukipita karibu na shule hiyo Wanafunzi hao walikuwa wamesimama juu ya shimo hilo lenye urefu wa takribani […]

WAKAZI WA KAPSABET WAOMBA UPANUZI WA BARABARA

Serikali imetakiwa kuchukua hatuza haraka na kupanua barabara kuu ya Kapsabet kaunti ya Nandi kuelekea Chavakali kaunti ya Vihiga, ili kuzuia visa vya ajali vinavyohusishwa na hali mbovu ya barabara hiyo. Wakizungumza mjini Kapsabet, wakazi, madereva na wahudumu wa boda boda wamelalamikia madai ya barabara hiyo kutelekezwa na idara husika, wakisema ni nyembamba mbali na […]

MAHAKAMA YASIMAMISHA FAINI ZA PAPO HAPO

Waendeshaji magari nchini wamepata afueni baada ya mahakama kuu kusimamisha utekelezaji wa mfumo wa mamlaka ya usalama barabarani, NTSA, kuwatoza faini za papo hapo wanapovunja sheria za trafiki. Kwenye uamuzi mapema leo, jaji Bahati Mwamuye ameizuia NTSA na afisi ya mwanasheria mkuu dhidi ya kutekeleza mfumo wa kuwatoza faini waendeshaji magari kwa njia yoyote ile […]

EACC, NG-CDF ZAJADILI KUZIBA UFISADI

Katika juhudi za kuziba mianya ya ufujaji wa fedha za umma katika hazina za kustawisha maeneo bunge, NG-CDF, tume ya maadili na kukabili ufisadi EACC inafanya kikao na maafisa wa NG-CDF kutoka magharibi mwa nchi. Mkutano huo unafanyika jijini Nakuru, mratibu wa EACC ukanda wa Magharibi Eric Ngumbi, akisema lengo ni kusaka suluhu kwa mianya […]

REAL WAITIA CITY KIKAONGONI, CHELSEA WAJIDHALILISHA UGENINI

Federico Valverde alifunga mara 3 na kuipa Real Madrid ushindi wa kushtua wa mabao 3-0 dhidi ya Manchester City, kwenye mkondo wa kwanza wa raundi ya 16 ya ligi ya klabu bingwa barani Ulaya. Vijana hao wa Alvaro Arbeloa walilipiza kisasi cha kichapo walichopokezwa Disemba mwaka jana katika uwanja huo wa Santiago Bernabeu, na kujiweka […]

MABINGWA WA SHULE KAKAMEGA WADUMISHA UBINGWA

Shule za Butere Girls na Musingu Boys zilidumisha ubingwa wao wa michezo ya shule za upili katika kaunti ya Kakamega, baada ya mashindano hayo kukamilika hapo jana. Butere Girls maarufu kama Cannons walikosa adhabu kabisa na kuwalaza Eregi Girls 122-26 katika mchezo wa vikapu, hali iliyoonekana kama kutoa onyo kwa wapinzani wao katika kiwango cha […]

MAADHIMISHO YA NAKURU RFC YAVUTIA MAKUMI YA TIMU

Zaidi ya timu 40 za mchezo wa raga zimeratibiwa kushiriki mashindano ya 10-aside yatakayoandaliwa na kalbu ya Nakuru RFC mapema mwezi ujao, klabu hiyo itakapokuwa ikiadhimisha miaka 100 tangu kuanzishwa kwake. Klabu hiyo imehusishwa na mchango wake mkubwa kwa raga ya Kenya, ikiwemo kuwatoa wachezaji mahiri wanaochezea timu ya taifa. Mashindano hayo huandaliwa kila mwezi […]

AFUENI YA KILIMO BUNGOMA

Wakulima 22,500 wa mapato ya chini katika kaunti ya Bungoma wamepata afueni msimu huu wa upanzi baada ya kupokezwa mbegu za mahindi na mbolea, ikiwa ni sehemu ya serikali ya kaunti hiyo kuimarisha uzalishaji wa chakula cha kutosha. Kulingana na gavana wa kaunti hiyo Ken Lusaka, mpango huo unalenga kuwaimarisha wakulima hao ili kukabiliana na […]

USHAURI WA NATEMBEYA KWA IEBC

Wakati uo huo, gavana wa Trans Nzoia George Natembeya, ametoa changamoto kwa tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC kutumia uchaguzi mkuu ujao kurejesha imani ya wakenya, kwa kuhakikisha uwazi uhuru na haki katika matokeo hasa ya urais. Kwenye mahojiano na kituo kimoja cha runinga, gavana huyo amesema kuwa wakenya wamekosa imani kwenye tume hiyo […]