NGATIARI NA NJERI WANG’ARA MIGA GOLF CLUB
Anthony Ngatiari na Teresia Njeri wameibuka washindi wakuu katika duru ya 10 ya Mfululizo wa Gofu wa NCBA 2026 iliyofanyika katika Migaa Golf Club mwishoni mwa wiki, huku mbio za kufuzu fainali kuu zikiendelea kushika kasi.
Katika kitengo cha Wanaume, Ngatiari alionyesha mchezo wa kiwango cha juu na kutwaa nafasi ya kwanza katika kundi lililokuwa na zaidi ya wachezaji 100, akionekana kudhibiti mashindano kwa umakini mkubwa.
Kwa upande wa wanawake, Teresia Njeri aliibuka mshindi wa jumla akiwa na alama 75 nett, huku Agnes Wairimu akishika nafasi ya pili baada ya kupata alama 81 nett, katika mashindano hayo yanayoelekea fainali kuu itakayofanyika Novemba katika Karen Country Club.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 














































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































