WANAFUNZI WA UON WATISHIA MGOMO KUHUSU MAKAMU CHANSELLA
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Nairobi wametishia kugoma wakidai kuteuliwa kwa Makamu Mkuu wa chuo hicho.
Wanafunzi hao wanasema kucheleweshwa kwa uteuzi huo kumeathiri uongozi na uendeshaji wa chuo, hali wanayodai inasababisha sintofahamu miongoni mwa wanafunzi na wahadhiri.
Wameonya kuwa watachukua hatua za mgomo iwapo suala hilo halitashughulikiwa haraka na mamlaka husika.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 














































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































