#Local News

RUTO AWATAKA MAJAJI KUDUMISHA UADILIFU

Rais William Ruto amewataka majaji wapya kudumisha uadilifu, uhuru na ufanisi katika utoaji wa haki.

Akizungumza wakati wa hafla ya kuapishwa kwa Majaji 37 wa mahakama mbalimbali, Rais amesema jukumu kuu la mahakama ni kulinda katiba na haki za wananchi, akisisitiza kuwa mamlaka yao yanatokana na katiba na yanapaswa kutekelezwa kwa mujibu wa sheria.

Aidha, amewakumbusha kuwa maamuzi yao yanapaswa kuongozwa na ushahidi na sheria pekee, huku akionya kuwa ucheleweshaji wa kesi mahakamani hudhoofisha imani ya umma katika taasisi za haki.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *