POLICE BULLETS YALENGA UBINGWA WA TATU MFULULIZO
Kocha wa Kenya Police Bullets David Vijago amesema ana imani hakuna kitakachowazuia kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake kwa mara ya tatu mfululizo.
Timu hiyo ilithibitisha ubora wake baada ya kuichapa Vihiga Queens mabao 9–0 katika uwanja wa Police Sacco, huku Margaret Kunihira na Emily Moranga wakifunga mabao mawili kila mmoja, na wenzao kuchangia mabao yaliyosalia.
Ushindi huo umeiweka kileleni ikiwa na pointi 49, ikifuatiwa na Ulinzi Starlets kwa tofauti ya pointi mbili, huku timu nyingine zikiendelea kushindania nafasi za juu kwenye jedwali la ligi.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































