#Football #Sports

JUNIOR STARLETS YATAJA KIKOSI CHA AWALI

Kocha wa Junior Starlets Mildred Cheche ametaja kikosi cha awali cha wachezaji 30 kuelekea mechi za kufuzu Kombe la Dunia kwa wasichana chini ya miaka 17 dhidi ya Uganda.

Cheche amedumisha sehemu kubwa ya kikosi kilichofanya vyema katika raundi iliyopita ambapo waliifunga Namibia kwa jumla ya mabao 7–1 na kufuzu hatua inayofuata.

Kikosi hicho kinatarajiwa kuripoti kambini tarehe 6 Mei  katika uwanja wa Kasarani Annex, ambapo wachezaji 23 wa mwisho watachaguliwa kabla ya mechi hiyo muhimu.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *