CHERARGEI AWASILISHA HOJA YA KUSITISHA MARUPURUPU YA UHURU
Seneta wa Nandi Samson Cherargei amewasilisha hoja katika Seneti akitaka kusitishwa au kupunguzwa kwa marupurupu ya Rais mstaafu Uhuru Kenyatta.
Kupitia hoja hiyo, Cherargei anataka Bunge kufuta, kubadili au kugawa upya fedha zinazohusiana na marupurupu ya kiongozi huyo wa zamani, akipendekeza fedha zitakazookolewa zielekezwe kwa maslahi ya wananchi.
Hatua hiyo inajiri wakati washirika wa Rais William Ruto wakiendelea kumkosoa Uhuru kutokana na msimamo wake wa kisiasa.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 














































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































