RUTO: UDA-ODM BADO PAMOJA

Rais William Ruto amekariri kuwa vyama vya UDA na ODM vitaendelea kushirikiana kupitia mpango wa serikali jumuishi yaani Broad-based ili kufanikisha mageuzi nchini. Kulingana na Ruto, ni kupitia ushirikiano huo ndipo wananchi katika maeneo mbali mbali watafikiwa na maendeleo, akiwaonya viongozi wa upinzani dhidi ya kauli zao anazosema zitalitumbukiza taifa katika machafuko. Amehimiza ukomavu wa […]

MAN U MBIONI KUTAFUTA USHINDI DHIDI YA LEEDS

Manchester United wapo mbioni kujiweka katika nafasi nzuri watakapomenyana na Leeds United kwenye uwanja wa Old Trafford. Mechi ya mkondo wa kwanza iliishia sare ya bao 1-1 united wakiwa chini ya Ruben Amorim lakini wameonyesha mchezo mzuri chini ya Kocha wa Muda Michael Carrick na sasa timu hiyo inatazamiwa kupata ushindi. Ushindi kwa united kutawaweka […]

LIVERPOOL YAKABILIWA NA KIBARUA KIGUMU ULAYA

Liverpool wanakabiliwa na kibarua kigumu kuondoa mabingwa watetezi Paris Saint-Germain katika mashindano ya klabu bingwa Ulaya, lakini wanatumai uwanja wao wa nyumbani utawapa matumaini mapya. Timu hiyo kwa sasa inashika nafasi ya tano katika msimamo wa ligi ya Uingereeza na imeshindwa kufanya vyema katika mashindano ya ndani, hivyo mashindano ya Ulaya yamebaki kuwa nafasi yao ya mwisho […]

BANDARI YALENGA UBINGWA WA KOMBE LA FKF

Kocha wa makipa wa Bandari Razak Siwa, ameihimiza timu yake kuongeza bidii wanapolenga kutwaa Kombe la Shirikisho la Soka nchini na kujipatia nafasi ya kushiriki mashindano ya vilabu barani Afrika msimu ujao. Siwa amesema wana uwezo wa kurudia mafanikio ya mwaka 2015 walipotwaa kombe hilo, akiongeza kuwa chini ya kocha mkuu Bernard Mwalala, timu hiyo […]

NEKESA AAPA USHINDI KABLA YA MECHI DHIDI YA AUSTRALIA

Mshambuliaji wa Harambee Starlets, Valerie Nekesa, amesema haogopi mechi ya fainali dhidi ya Australia katika michuano ya Fifa Global Series itakayofanyika kwenye Uwanja wa Nyayo. Nekesa amesema nafasi za viwango vya ubora duniani hazitakuwa na maana wakati timu hizo zitakapoingia uwanjani, akisisitiza kuwa kila timu itakuwa na nafasi sawa ya ushindi. Mechi hiyo inatazamwa kuwa […]

VOLIBOLI: TIMU ZA KENYA ZAPANGIWA MAKUNDI MAZITO AFRIKA

Timu za juu za mpira wa wavu wa wanawake nchini Kenya zimepata wapinzani wao kufuatia droo ya Mashindano ya Klabu Bingwa Afrika mjini Cairo, Misri. Kenya Pipeline wamewekwa Kundi B wakikutana na timu kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Senegal, Ghana na Burundi, huku DCI Queens wakipangwa Kundi C pamoja na timu kutoka Tunisia, Nigeria, […]

WETANG’ULA AONYA KUHUSU UKOSEFU WA UVUMILIVU KISIASA

Spika wa Bunge la Taifa Moses Wetang’ula ameonya kuhusu kuongezeka kwa ukosefu wa uvumilivu wa kisiasa, akisema hali hiyo inatishia demokrasia kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2027. Wetang’ula amesema vurugu na kuvurugwa kwa mikutano ya umma na makundi ya wahuni vinaweza kudhoofisha imani ya wananchi katika mchakato wa uchaguzi iwapo hatua hazitachukuliwa. Akizungumza katika ibada […]

POLISI WACHUNGUZA KIFO CHA MTOTO MTAANI BURUBURU

Polisi katika jiji la Nairobi wameanzisha uchunguzi kuhusu kifo cha mtoto wa miaka tisa kilichotokea katika eneo la Buruburu chini ya mazingira yasiyoeleweka. Kwa mujibu wa polisi, mtoto huyo ambaye alikuwa mwanafunzi wa Gredi ya kwanza katika Shule ya Msingi ya Kaloleni alitoka nyumbani tarehe kumi Aprili majira ya saa nne asubuhi kwenda kucheza kabla ya kurejea […]

UASU YATAKA SULUHU YA MGOGORO CHUO KIKUU CHA NAIROBI

Chama cha Wahadhiri wa Vyuo Vikuu, tawi la chuo cha kikuu cha Nairobi, kimetoa onyo kali kuhusu kile kinachodaiwa kuwa mgogoro wa uongozi na fedha unaozidi kuongezeka katika chuo hicho. Katika taarifa, chama hicho kimeeleza wasiwasi kuhusu ukosefu wa uongozi wa kudumu, kikibainisha kuwa nafasi za Naibu chansella na wasaidizi wake zimekuwa zikishikiliwa kwa muda tangu Septemba mwaka […]

WANDAYI AHOJIWA KUHUSU MAFUTA DUNI

Waziri wa Kawi Opiyo Wandayi amehojiwa na kamati ya bunge kuhusu madai ya uagizaji wa mafuta ya viwango duni nchini. Kamati hiyo imeanza uchunguzi wa kina kubaini namna mafuta hayo yaliingizwa nchini na hatua zilizochukuliwa dhidi ya waliohusika katika kashfa hiyo. Wandayi amesema mafuta hayo yalirudishwa na kusisitiza kuwa ndiye aliyemuarifu Rais William Samoei Ruto […]