#Local News

MAWAKILI DEBENI KUWACHANGUA VIONGOZI WA LSK

Uchaguzi wa viongozi wapya wa chama cha wanasheria nchini LSK umeanza rasmi asubuhi, uchaguzi ambao huenda ukatoa mwelekeo mpya wa chama hicho.

Mawakili wamejitokeza katika vituo vilivyoteuliwa vya kupigia kura, uchaguzi huo ukiandaliwa katika kipindi ambacho LSK imekuwa na nafasi kubwa katika kuhakikisha uongozi bora, uzingatiaji wa katiba na utawala wa sheria.

Miongoni wanaowania wadhifa wa Rais wa LSK ni Peter Wanyama, wakili Charles Kanjama na Mwaura Kabata.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *