AFISA WA ZAMANI WA KMPDC AKAMATWA KISA SHA
Maafisa wa DCI wamemkamata aliyekuwa mfanyakazi wa KMPDC, Harun Liluma, kuhusiana na tuhuma za ulaghai unaoathiri Social Health Authority (SHA).
Liluma anakabiliwa na mashtaka ya kula njama ya kutapeli, matumizi mabaya ya ofisi, kuingia bila idhini kwenye mifumo ya kompyuta na ulaghai wa kimtandao.
Waendesha mashtaka wanadai kuwa Liluma alitumia nafasi yake KMPDC kuwezesha usajili usio halali na malipo kwa vituo kadhaa vya afya, hatua iliyowaruhusu kudai fedha kutoka SHA kwa misingi ya uongo.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 













































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































