#Local News

BABU AASHIRIA KUANZISHA CHAMA KIPYA CHINI YA LINDA MWANANCHI

Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino amedokeza uwezekano wa kuanzishwa kwa chama kipya cha kisiasa chini ya vuguvugu la “Linda Mwananchi,” akionyesha mabadiliko yanayoweza kujitokeza kuelekea uchaguzi mkuu wa 2027.

Akizungumza katika mahojiano, Babu amesema Wakenya wanapaswa kutarajia chama kipya chenye mwelekeo na uongozi tofauti, akionekana kujitenga na chama chake cha sasa cha ODM.

Aidha, mbunge huyo ametangaza nia yake ya kuwania kiti cha ugavana wa Nairobi, akisisitiza kuwa atafanya hivyo kupitia chama cha kisiasa na si kama mgombea huru.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *