#Local News

WANAFUNZI WA UON WATISHIA MGOMO KUHUSU MAKAMU CHANSELLA

Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Nairobi wametishia kugoma wakidai kuteuliwa kwa Makamu Mkuu wa chuo hicho.

Wanafunzi hao wanasema kucheleweshwa kwa uteuzi huo kumeathiri uongozi na uendeshaji wa chuo, hali wanayodai inasababisha sintofahamu miongoni mwa wanafunzi na wahadhiri.

Wameonya kuwa watachukua hatua za mgomo iwapo suala hilo halitashughulikiwa haraka na mamlaka husika.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *