#Local News

UHURU ALENGWA KUPOKONYWA MANUFAA

Mswada wa kumpkonya Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta marupurupu yake umeratibiwa kuwasilishwa leo katika bunge la seneti, Kenyatta akituhumiwa kuendelea kujihusisha na siasa licha ya kustaafu.

Mswada huo umefadhiliwa na seneta wa Nandi Samson Cherargei, anayesisitiza kuwa ni ukiukaji wa sheria kwa Kenyatta kuendelea kuikosoa serikali, hatua hii ikijiri baada ya rais huyo wa zamani kuishutumu serikali kwa madai ya kulenga kumnyima haki ya kujieleza kisiasa.

Hata hivyo, chama cha Jubilee kimepinga mswada huo.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *