#Football #Sports

USIKU MKUBWA WA ARSENAL

Katika kinachoonekana kuwa tukio kubwa zaidi katika historia ya uwanja wa Emirates, Arsenal itakuwa mwenyeji wa Atletico Madrid katika mkondo wa pili wa mechi ya semi fainali ya klabu bingwa bara Ulaya, wanapolenga kucheza fainali ya mashindano hayo kwa mara ya kwanza tangu ufunguzi wa uwanja huo mwaka wa 2006.

Viktor Gyokeres na Julian Alvarez walifunga mikwaju ya penalti katika sare ya bao 1-1 kwenye mechi ya mkondo wa kwanza jijini Madrid, na kuacha mlango wazi kwa timu yoyote kufuzu fainali hizo jijini Budapest mwishoni mwa msimu.

Arsenal hawajapoteza mechi yoyote katika mechi 13 za klabu bingwa bara Ulaya msimu huu, zikiwemo 5 kati ya 6 walizocheza uwanjani humo, na watalenga kutumia rekodi hiyo kupata ushindi.

Mshindi wa pambano la leo atakabiliana na mshindi wa pambano la hapo kesho kati ya bingwa mtetezi PSG, na miamba wa Ujerumani Bayern Munich.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *