#Football #Sports

ARSENAL WAFAIDI HASARA YA CITY DHIDI YA EVERTON

Bao la Wing’a Jeremy Doku katika dakika za mwisho lilinusuru pointi moja kwa Manchester City katika sare ya mabao 3-3 dhidi ya Everton, sare ambayo imewaacha Arsenal wakiwa wameshikilia usukani wa taji la ligi kuu ya soka nchini Uingereza, EPL.

Arsenal walio na pointi 76, 5 mbele ya City, sasa watahitaji kushinda mechi zao zote 3 zilisolia kutawazwa mabingwa bila kutatizwa na wingi wa mabao.

Vijana wa Pep Guardiola waliidhibiti mechi ya jana usiku ugani Hill Dickinson, wakikosa nafasi za wazi katika kipindi cha kwa kilichokamilika wakiwa mbele bao 1-0 walilofungiwa na Doku.

Hata hivyo, safu ya ulinzi iliporomoka chini ya shinikizo za Everton, na makosa ya mabeki wa kati Abdukodir Khusanov na Marc Guehi yakatishia kuwapokonya ligi.

Makosa hayo yaliidhabiwa na wenyeji wao na kuwafunga mabao 3 ya haraka, kabla ya Erling Haaland na Doku kujibu upesi na kuokoa alama moja.

 Katika matokeo mengine, matumaini ya Chelsea kupata tiketi ya kufuzu mashindano ya bara Ulaya msimu jana yalididimia, baada ya kudhalilishwa kwa kichapo cha mabao 3-1 na Nottingham Forest.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

ARSENAL WAFAIDI HASARA YA CITY DHIDI YA EVERTON

USIKU MKUBWA WA ARSENAL

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *