ODM YAITISHA MKUTANO MAALUM WA WAJUMBE NAIROBI

Chama cha ODM, kimeitisha mkutano maalum wa wajumbe utakaofanyika Machi 27 mwaka huu katika Kaunti ya Nairobi. Kwa mujibu wa taarifa ya chama hicho, mkutano huo utawakutanisha viongozi wa juu wa chama wakiwemo wajumbe wa Kamati Kuu ya Kitaifa, Kundi la Wabunge pamoja na wawakilishi kutoka miundo ya chama katika kaunti mbalimbali. Mkutano huo pia utahudhuriwa na wenyeviti […]

MJANE WA NG’ENO AAHIDI KUWAHUDUMIA WANANCHI

Mjane wa aliyekuwa Mbunge wa Emurua Dikirr Johanna Ng’eno, Naiyanoi Ntutu, ameapa kuendelea kusimama na wananchi wa eneo hilo hata baada ya kifo cha mumewe. Akizungumza wakati wa ibada ya mazishi, Naiyanoi amewashukuru wakazi wa Emurua Dikirr kwa upendo na msaada waliouonyesha familia yake katika kipindi cha maombolezo. Aidha, Amesema ataendelea kuwahudumia wananchi kama alivyofanya marehemu mumewe, […]

WAFUASI WA NATEMBEYA WATEMBEA NAYE BUNGOMA

Uamuzi wa mahakama kumwondolea mashtaka ya ufisadi gavana wa Trans Nzoia George Natembea umeendelea kushabikiwa na wafuasi wake katika kaunti jirani ya Bungoma, wakiutaja uamuzi huo kuwa ushindi kwa umma. Wakiongoza maandamano ya amani mjini Bungoma, wafuasi hao wameitaka tume ya maadili na kukabili ufisadi EACC kufanya uchunguzi wa kina kabla ya kuwakamata viongozi kuhusiana […]

IEBC YAONYA KUHUSU UTAPELI WA AJIRA

Tume huru ya uchaguzi na mipaka, IEBC, imetoa tahadhari kwa umma kuhusiana matangazo ya ulaghai yanayosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu nafasi za ajira katika tume  hiyo. Kupitia tangazo, IEBC imefafanua kwamba matangazo hayo ni ya udanganyifu, na kusisitiza kwamba nafasi za ajira katika tume hiyo hutolewa tu kupitia tovuti yake rasmi. Imewataka wakenya kuwa […]

UTOAJI WA CHANJO YA ROTAVIRUS KUTATIZIKA

Wizara ya afya imetangaza kwamba utoaji wa chanjo za rotavirus zinazotumiwa kwa chanjo ya kawaida ya Watoto utatatizika kwa muda kutokana na uhaba wa chanjo hizo nchini. Kupitia tangazo, Waziri wa afya Aden Duale, amefichua uhaba wa chanjo hizo, ambazo hutolewa kwa Watoto wanapofikisha umri wa wiki 6, 10 na 14, shehena ya chanjo hizo […]

RUTO AHUDHURIA MAZISHI YA MBUNGE NG’ENO

Rais William Ruto ni miongoni mwa viongozi mashuhuri na waombolezaji wengine wanaohudhuria hafla ya mazishi ya mbunge wa Emurua Dikirr Johanna Ng’eno, na watu wengine 4 katika eneo la Mogondo. Wanne hao ni mwalimu Wycliffe Rono, Amos Kiprotich, Robert Kipkoech na Nicholas Kosgey ambao hafla yao ya mazishi inaandaliwa kwa pamoja katika shule ya msingi […]

BENKI YA DUNIA YATENGA KES. 64 KUBORESHA RELI YA TRENI YA ABIRIA NAIROBI 

Benki ya Dunia inatazamiwa kutumia takriban shilingi bilioni 64.5 kusaidia ukarabati wa njia ya reli ya abiria jijini Nairobi kama sehemu ya mpango mpana wa kuboresha usafiri wa mijini katika mji mkuu. Kufuatia ripoti, mpango huo kwa sasa uko katika hatua ya kukagua dhana na ni sehemu ya mpango mkubwa unaokadiriwa kugharimu takriban shilingi bilioni 219. Kulingana na dokezo la mradi […]

FA CUP RAUNDI YA 5 KUNG’OA NANGA USIKU

Kipute cha FA nchini Uingereza kinaingia raundi ya tano wikendi hii, huku mechi ya kwanza ikisakatwa leo usiku. Kwenye mechi hiyo, Wolves wanaialika Liverpool katika uwanja wa Molineux, takribani siku 3 baada ya kuwachapa wekundu hao wa Anfield kichapo cha mabao 2-1 kwenye mechi ya ligi kuu. Kocha mkuu wa Wolves Rob Edwards, alifanya mageuzi […]

LIGI KUU YA KENYA KUCHUKUA BREKI KUPISHA FKF CUP

Mechi za ligi kuu ya Kenya, KPL, zitachukua mapumziko wikendi hii ili kupisha mechi za raundi ya 32 za kuwania ubingwa wa FKF Cup. Mechi ya mwisho ya wiki ya KPL ilichezwa hapo jana ambapo Gor Mahia walilazimisha sare ya bao 1-1 dhidi ya Posta Rangers, na kuongeza pengo la uongozi kileleni kwa pointi 7 […]

WAFCON 2026 YAAHIRISHWA

Dimba la taifa bingwa barani Afrika la wanawake mwaka huu, WAFCON 2026 limeahirishwa, zikiwa zimesalia siku 11 kabla ya tarehe iliyokuwa imeratibiwa kuanza kwa mashindano hayo. Kupitia taarifa, shirikisho la soka barani Afrika, CAF, limesema Makala ya mwaka huu yataandaliwa mwezi Julai kutokana na kile ambacho limetaja kwamba sababu zisizoweza kutabirika. Makala ya mwaka huu […]