EPL: ARSENAL KUPIMANA NGUVU NA CHELSEA
Ligi kuu ya uingereza itarejelewa tena kuanzia hii huku mechi kadhaa zikiratibiwa kuchezwa, Leo mwendo wa saa tano usiku Wolves watakua nyumbani kukaribisha Aston Villa. Siku ya kesho itashuhudia mechi kadhaa wakati Sunderland wakimenyana na Bournemouth mwendo wa saa tisa unusu, baadaye saa kumi na mbili Liverpool watakaribisha Westham, Newcastle wamenyane na Everton, Burnley wakabane koo na Brentford kisha Manchester City wapambane na Leeds United saa mbili unusu usiku. Siku ya Jumapili, Manchester United watakua nyumbani Old Trafford kuvaana na Crystal Palace, Fulham wakaribishe Tottenham, Kisha Brighton wapambane na Nottingham Forest Mechi zote zikichezwa saa kumi na moja jioni. Mechi inayosubiriwa kwa hamu itakua mwendo wa saa moja unusu wakati Arsenal wakikaribisha Chelsea kwenye London Derby mchezo ambao lazima Arsenal washinde ili kujiweka nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa wa EPL.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 




















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































