#Local News

MIRADI ITAKAYOFADHILIWA NA HAZINA YA MIUNDOMBINU…

Bunge la kitaifa limefafanua miradi itakayofadhiliwa na hazina ya kitaifa ya miundombinu ya shilingi trilioni 5, likisema ni miradi mikuu kama vile barabara kuu za kitaifa, miundombinu ya reli, viwanja vya ndege, bandari, uzalishaji wa umeme na na usambazaji.

Hii ni kufuatia kupitishwa kwa mswada wa hazina hiyo hapo jana baada ya marekebisho kadhaa, afisi ya Rais na bunge zikipewa mamlaka zaidi ya udhibiti wa hazina hiyo ambayo wabunge wanasema itafanikisha azma ya Rais William Ruto kuifanya Kenya iwe kama Singapore.

Kutokana na kupitishwa kwa mswada huo unaosubiri sahihi ya Rais kuwa sheria, wabunge wameonyesha matumaini ya kuboreshwa kwa miundombinu ya usafiri.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

MIRADI ITAKAYOFADHILIWA NA HAZINA YA MIUNDOMBINU…

DUALE: SHA INAWAHUDUMIA WALIMU

MIRADI ITAKAYOFADHILIWA NA HAZINA YA MIUNDOMBINU…

WAFCON 2026 YAAHIRISHWA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *