SHARKS WATOKA HATARINI FKF

Kocha wa Kariobangi Sharks William Muluya amesema ushindi wao wa bao 1–0 dhidi ya Ulinzi Stars ni afueni kubwa baada ya kipindi kigumu walichopitia wakisalia mkiani mwa jedwali la Ligi Kuu ya FKF. Ushindi huo umevunja mfululizo wa mechi tano bila ushindi kwa Sharks na kuwainua kutoka eneo la kushuka daraja. Bao pekee la mechi […]

TAHARUKI YAJITOKEZA CBD NAIROBI

Taharuki imeshuhudiwa katika eneo la biashara katikati ya jiji la Nairobi, CBD, baada ya polisi kuingilia kati maandamano ya wahudumu wa magari ya uchukuzi wa umma. Maafisa wa polisi wameonekana wakiondoa vizuizi barabarani na kung’oa nambari za magari ya matatu yaliyokuwa yameegeshwa katika barabara kuu, huku wakijaribu kurejesha hali ya kawaida ya usafiri jijini. Maandamano hayo […]

OBURU: ODM ITAENDELEA KUSHIRIKIANA NA UDA

Kiongozi wa chama cha ODM na Seneta wa Siaya Oburu Odinga amesema kuwa chama hicho kitaendelea kushirikiana na UDA, huku kikitarajia kuendeleza mazungumzo na serikali kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2027. Akizungumza wakati wa hafla ya utoaji wa fedha za NYOTA jijini Kisumu Oburu amesifu uhusiano kati ya ODM na UDA ndani ya serikali jumuishi, akisema […]

OSOTSI ATAKA ODM ISIMAMISHE MGOMBEA 2027

Seneta wa Vihiga Godfrey Osotsi amekitaka chama cha ODM kusimamisha mgombea urais katika Uchaguzi Mkuu wa 2027, akipinga vikali mapendekezo kwamba chama hicho kijiunge na kumuunga mkono Rais William Ruto. Akizungumza kuhusu mustakabali wa chama hicho baada ya kifo cha aliyekuwa kiongozi wake wa muda mrefu Raila Odinga, Osotsi amesema ODM bado ni chama imara […]

MRADI WA NYOTA WAZINDULIWA KISUMU

Rais William Ruto ameongoza uzinduzi wa Mradi wa NYOTA jijini Kisumu, unaolenga kuwawezesha vijana kiuchumi kwa kuwapatia mtaji wa kuanzisha biashara ndogondogo. Chini ya mpango huo, vijana wanapokea ruzuku ya shilingi 25,000 kila mmoja kama mtaji wa kuanzisha au kupanua biashara zao, ikiwa ni sehemu ya juhudi za serikali kupunguza ukosefu wa ajira miongoni mwa […]

SALASYA AONDOLEWA MASHTAKA BAADA YA KUTII MAHAKAMA

Mahakama ya Milimani jijini Nairobi imemwondolea kesi ya uchochezi mbunge wa Mumias East Peter Salasya baada ya mbunge huyo kutii maagizo ya mahakama yaliyomtaka afanye kampeni za kuhubiri amani kote nchini. Akitoa uamuzi huo, hakimu Paul Mutai, ameamuru kwamba Salasya amewafikia zaidi ya watu 1,000 kwenye kampeni hizo, ikiwemo mipango ya kampeni inayoendelea kwenye mitandao […]

MAHAKAMA YAWAAGIZA MADAKTARI WA KONGO, WIZARA KUELEWANA

Mahakama kuu imeziagiza pande husika katika mzozo unaowahusisha madaktari raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wanaohudumu nchini na wizar ya afya kutatua mgogoro huo kupitia mazungumzo, kufuatia mwasilisho wakati wa kutajwa kwa kesi hiyo. Kesi hiyo imetajwa mbele ya jaji Roseline Aburili, ambako madaktari hao wapatao 50, wanapinga wanachokitaja kama uamuzi wa kiholela na […]

MAHAKAMA KUU YABATILISHA NYONGEZA YA MALIPO ILIYOIDHINISHWA NA SRC

Mahakama Kuu ya Milimani imetangaza kuidhinishwa na Tume ya Mishahara na Marupurupu (SRC) ya nyongeza ya mishahara kwa watumishi wa umma kwa mwaka wa fedha wa 2023/2024 na 2024/2025 kuwa kinyume na katiba. Jaji Lawrence Mugambi aliamua kwamba nyongeza za mishahara zilitekelezwa bila ushiriki wa kutosha wa umma na kukiuka matakwa ya kikatiba kuhusu uwajibikaji […]

Free Slot Games Online There are a variety of options to play free online slots. A casino on the internet is the best choice. These casinos are known for offering many games. In addition, they will provide you with the most popular machines and their bonus features. They also provide information about the different types […]

CARRICK AENDELEZA REKODI MURWA

Meneja mshikilizi wa Manchester United, Michael Carrick, aliendeleza rekodi yake ya ushindi, tangu kuchukua hatamu za klabu hiyo kutoka kwa Ruben Amorim, sasa akiwa na ushindi katika mechi 3 mfululizo. Bao la Benjamin Sesko katika dakika za majeruhi zilizima uasi wa Fulham waliotishia kuwapokonya United alama, na kuishia katika ushindi wa mabao 3-2. United walichukua […]