SIFUNA APATA MWANGA MPYA
Katibu mkuu wa ODM na ambaye ni seneta wa Nairobi Edwin Sifuna, amepata afueni ya muda kufuatia uamuzi mpya wa jopokazi la kutatua migogoro ya vyama vya kisiasa kwamba hatua zozote za kumtimua kutoka wadhifa wa chama hicho usitishwe hadi kesi aliyowasilisha itakaposikilizwa na kuamuliwa.
Akitoa agizo hilo, kaimu mwenyekiti wa jopokazi hilo Gad Gathu, amesema licha ya ODM kuwa na uhuru wa kuendelea na mchakato wa kumwadhibu Sifuna, uamuzi wao haufai kutekelezwa hadi kesi hiyo iamuliwe.
Kesi hiyo itasikilizwa tarehe 9 mwezi ujao.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 







































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































