FELIX OLOO AFARIKI KATIKA AJALI MAREKANI
Kocha wa zamani wa Kenya Lionesses na mchezaji wa zamani wa Nakuru RFC Felix Oloo amefariki dunia baada ya kuhusika katika ajali mbaya ya barabarani nchini Marekani.
Inaripotiwa kuwa Oloo aligongwa na gari alipokuwa akijaribu kuvuka barabara kuu ya Interstate 405 katika eneo la Bothell, Washington, katika tukio lililotokea mapema Jumatatu asubuhi ambalo bado linachunguzwa.
Chama cha Nakuru RFC kimethibitisha kifo chake, kikieleza masikitiko makubwa kufuatia kifo hicho cha ghafla cha kocha na mchezaji huyo wa zamani wa raga nchini Kenya.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 




































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































