SIRAJ MOHAMMED ANG’ARA KCB
Uchezaji wa beki wa kushoto Siraj Mohammed akiwa katika klabu ya KCB umeendelea kuimarika, baada ya kipindi cha mkopo kilichompa nafasi ya kurejea katika kiwango chake cha juu.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27, anayefahamika kwa jina la utani “Mastermind,” alijiunga na KCB mwezi Februari 2026 baada ya kukosa nafasi ya kucheza katika klabu ya Gor Mahia, na tangu hapo ameonyesha uimara katika safu ya ulinzi.
Kocha wa KCB Robert Matano amesema amefurahishwa na nidhamu na juhudi za mchezaji huyo, akisisitiza kuwa amejitolea kujenga upya taaluma yake na kuchangia kikosi hicho kwa kiwango cha juu.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 




































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































