#Local News

OGAMBA AHIMIZA UTEKELEZAJI WA CBE

Waziri wa Elimu Julius Ogamba ametoa wito wa kuharakishwa kwa utekelezaji wa mfumo wa elimu unaozingatia ujuzi wa mwanafunzi, CBE.

Ogamba amesisitizaumuhimu wa mfumo huo katika kukuza ubunifu na kuwajengea wanafunzi ujuzi unaohitajika katika soko la ajira.

Wadau wa elimu pia wameitaka serikali kuunga mkono ubunifu na kuwekeza zaidi katika rasilimali na miundombinu ili kuhakikisha utekelezaji bora wa mfumo huo.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *