#Football #Sports

FODEN ASAINI MKATABA MPYA MANCHESTER CITY

Kiungo wa Manchester City Phil Foden amesaini mkataba mpya utakaomweka klabuni hapo hadi Juni 2030, huku makubaliano hayo yakithibitishwa rasmi.

Taarifa zinaeleza kuwa klabu hiyo imeonyesha imani kubwa kwa Foden, ambaye amekuwa mmoja wa wachezaji muhimu katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo.

Mkataba huo mpya pia unajumuisha kipengele cha kuongeza muda wa kuendelea hadi mwaka 2031, ikiwa makubaliano zaidi yatakamilishwa baadaye.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *