NATEMBEYA AIBUKA MAARUFU MAGHARIBI

Ulingo wa kisiasa Magharibi mwa Kenya umechukua mkondo tofauti, utafiti ukionyesha kuwa wenyeji sasa wamewaasi viongozi wa siku nyingi eneo hilo na kuwakumbatia viongozi wa kizazi kipya. Kulingana na matokeo ya utafiti wa shirika la Infotrak yaliyotolewa hapo jana kuhusu umaarufu wa viongozi wa eneo hilo, gavana wa Trans Nzoia George Natembeya anapendelewa na asilimia […]

MUDAVADI AITETEA SERIKALI KUHUSU WAKENYA URUSI

Wakenya wengi waliohadaiwa kuhusu nafasi za ajira nchini Urusi na kisha kujipata katika vita kati ya taifa hilo na Ukraine hawakutoa taarifa kwa serikali kuhusu maelezo ya kazi waliozitiwa na safari zao kuelekea Urusi. Haya ni kwa mujibu wa mkuu wa mawaziri Musalia Mudavadi, akiitetea serikali dhidi ya madai ya kushindwa kuwalinda raia wake dhidi […]

ASILIMIA KUBWA YA WAKENYA WANANUNUA BIDHAA KWENYE PROGRAMU , MITANDAO YA KIJAMII

Programu za rununu na majukwaa ya mitandao ya kijamii, haswa WhatsApp, zimepita tovuti za kitamaduni kama njia kuu za biashara ya mtandaoni nchini, kufuatia uchunguzi uliofanywa na shirika la Mawasiliano nchini (CA). Kama ilivyoripotiwa, programu za simu zinachukua asilimia 44.8 ya maagizo ya mtandaoni, huku WhatsApp ikichangia asilimia 20.2, ikionyesha kuongezeka kwa biashara ya mazungumzo, […]

UCHUMI WA KENYA WAKUA KWA 4.9% ROBO YA TATU YA 2025

Shirika la kitaifa kuhusu takwimu (KNBS) limesema uchumi wa Kenya umeongezeka kwa asilimia 4.9 katika robo ya tatu ya mwaka 2025 ikilinganishwa na asilimia 4.2 ya mwaka 2024. Kwa mujibu wa KNBS, ukuaji huo unatokana na kuboreshwa kwa utendakazi wa sekta kadhaa muhimu, ikiwa ni pamoja na kilimo, uzalishaji viwandani na usafiri, ambapo sekta za […]

BARCA, REAL WAPATA “MTEREMKO” COPA DEL REY

Mabingwa watetezi wa taji la Copa del rey nchini Uhispania Barcelona, na miamba wa soka nchini humo Real Madrid watapambana na timu za kutoka divisheni ya pili kwenye awamu ya mwondoano ya taji hilo kutokana na droo ya hapo jana. Barcelona watachuana na Racing Snatander ugenini huku Real wakichuana na Albacete, timu nyingine za La […]

SESKO ATALETA MWANGA, FLETCHER

Kocha mshikilizi wa Manchester United Darren Fletcher ana matumaini kwamba mabao mawili yaliyofungwa na Benjamin Sesko katika sare ya mabao 2-2 dhidi ya Burnley jana usiku ni kiashiria cha kuimarika kwake baada ya kipindi kigumu kwa raia huyo wa Slovenia. Sesko alikuwa amefunga mara 2 pekee katika mechi 17 kabla ya jana tangu kuwasili kwake […]

GUARDIOLA APOTEZA TUMAINI EPL

Kocha mkuu wa Manchester City Pep Guardiola amekiri kuwa klabu hiyo haiwezi kufikiria kuipata Arsenal kileleni mwa ligi katika kinyanga’nyiro cha kusaka ubingwa wa ligi hiyo msimu huu baada ya msururu wao wa sare kufikia mechi 3 mfululizo. Licha ya Erling Haaland kuwaweka City kifua mbele kakatika kipindi cha kwanza jinsi ilivyofanyika dhidi ya Chelsea, […]

LEOPARDS WAREJEA UONGOZINI KPL

Miamba wa soka nchini AFC Leopards wamerejea uongozini mwa ligi kuu ya soka KPL kufuatia ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Nairobi United ugani Nyayo, na kupanda juu ya washikilizi wa rekodi ya ubingwa Gor Mahia kwa pointi 1. Naibois walijifunga bao kunako dakika ya 20 kabla ya Ingwe kufunga bao la pili kunako dakika […]

TRUMP: NITAIENDESHA VENEZUELA

Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza kuwa serikali yake itamwelekeza kikamilifu cha kufanya kiongozi wa muda wa Venezuela Delcy Rodriguez, ukiwemo uuzaji wa mafuta kwa muda usiojulikana baada ya kumbandua Nicolas Maduro. Kauli ya Trump inajiri huku Delcy akina kwamba hakuna utawala wan je unaoeindesha Venezuela Hata hivyo, Trump amesema Marekani italiendesha taifa hilo la […]

WANAFUNZI TRANS MARA SOUTH SHULENI

Hatimaye wanafunzi katika shule ya Sitet Comprehensive eneo la Trans Mara South wamepata fursa ya kurejea shuleni kwa muhula wa kwanza baada ya maafisa wa usalama kuwaondoa watu waliokuwa wakiishi kwenye shule hiyo. Operesheni hiyo iliongozwa na chifu wa Olodonyo-Orok Paul Rutto, mkurugenzi wa elimu eneo hilo George Muchina akiripoti kuwa wanafunzi wapatao 250 waliripoti […]