ODM YASISITIZA INGALI SERIKALINI
Chama cha ODM kimesisitiza kuwa kitaifanya mazungumzo ya kisiasa na vyama vye maono sawa kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka ujao, na kwamba hakitajiondoa serikalini jinsi baadhi ya viongozi wanavyodai.
Kumekuwa na tetesi kwamba ODM itajiondoa serikalini mwezi huu wakati wa mkutano wa wajumbe, ila kinara Oburu Oginga amezitaja tetesi hizo kama porojo.
IMetayarishwa na Antony Nyongesa
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































