AMBANI ATAKA INGWE KUJIAMINI ZAIDI KATIKA UBINGWA
Mwenyekiti wa AFC Leopards, Fred Ambani, amewataka wachezaji wake kupambana kwa nguvu katika mechi nane zilizosalia ili kufukuzia vinara Gor Mahia katika mbio za ubingwa.
Amesema hakuna nafasi ya kufanya makosa huku timu ikisaka kutwaa taji la ligi kwa mara ya kwanza baada ya takriban miaka 30, akisisitiza kuwa wanapaswa kushambulia na kukusanya pointi bila woga.
Leopards wako nafasi ya pili wakiwa na pointi 52, nne nyuma ya Gor Mahia, huku wakitarajiwa kukutana na Murang’a Seal Jumapili, wakati Gor wakicheza na Tusker. Kushindwa kwa Leopards katika mechi zilizosalia kunaweza kudhoofisha matumaini yao ya ubingwa.
Imetayarishwa na `Cyrus Sifuna
English 




































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































