#Local News

USAJILI WA MAKURUTU KUKUMBATIA AI

Mageuzi makubwa yanatarajiwa katika mfumo wa usajili wa makurutu wa kujiunga na idara ya polisi, serikali ikitangaza kutumia mfumo wa akiliunde, yaani Artificial Intelligence, AI, kuwasajili makurutu hao.

Kulingana na Waziri wa usalama wa kitaifa Kipchumba Murkomen, hatua hiyo inalenga kukiimarisha kikosi cha polisi kulingana na mageuzi ya kiteknolojia, akiongeza kuwa mfumo wa kidijitali utachukua mahala pa vitabu vya kunakili matukio katika vituo vya polisi, OB, kwa lengo la kupunguza ufisadi.

Umma utakuwa na fursa ya kupiga ripoti kwa polisi bila kuhitajika kufika vituoni.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

USAJILI WA MAKURUTU KUKUMBATIA AI

RUTO: REKODI YANGU ITANITETEA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *