MVUA KUBWA KUENDELEA, RIPOTI
Wakenya wamepewa tahadhari kuhusiana na mafuriko kutokana na mvua kubwa ambayo imebashiriwa kuendelea kunyesha katika maeneo mbali mbali ya nchi.
Katika ripoti yake ya hivi punde, idara ya utabiri wa hali ya anga imetangaza kuwa mvua hiyo itaendelea katika maeneo ya nyanda za juu za bonde la ufa, ukanda wa Ziwa Victoria, Pwani, nyanda za chini za Kusini Mashariki, Kaskazini mashariki pamoja na Kaskazini Magharibi.
Athari za mafuriko na maporomoko ya ardhi zimebashiriwa, umma ukitakiwa kuwa na uangalifu na kujiepusha na matukio ya kutembea au kuendesha magari katika barabara zilizofurika.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 




































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































