DCI YAWAKAMATA WASHUKIWA WAWILI WA UHALIFU TRANS NZOIA
Maafisa wa Idara ya Upelelezi wa Jinai DCI katika Kaunti ya Trans Nzoia wamewakamata watu wawili wanaoshukiwa kuhusika na uhalifu uliopangwa kufuatia operesheni ya kiusalama eneo hilo
Kupitia taarifa iliyotolewa, DCI imesema washukiwa hao walikamatwa katika msako ulioongozwa na taarifa za kijasusi uliofanywa na maafisa wa Kituo cha Polisi cha Kitale kwa kushirikiana na kikosi maalum cha upelelezi.
Operesheni hiyo ililenga maeneo ya Chebarus na Kibomet katika eneo la Trans Nzoia Magharibi, huku uchunguzi zaidi ukiendelea kubaini mtandao wa uhalifu unaohusishwa na tukio hilo.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 




































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































