#Local News

RUTO, SULUHU WASHUTUMIWA KWA KAULI

Kauli za Rais William Ruto na mwenzake wa Tanzania Samia Suluhu Hassan za kulenga kuwanyamazisha vijana wa kizazi cha Gen Z zimeibua shutuma katika ukanda wa Afrika Mashariki, wa hivi punde kushutumu kauli hizo akiwa jaji mkuu wa zamani David maraga.

Kwenye mazungumzo ya hadhara alipokuwa mwenyeji wa Ruto nchini Tanzania, Samia alikiri kushauriana na Ruto kuhusu jinsi ya kuwanyamazisha vijana hao aliowataja kuwa wasio na adhabu, akuli ambayo imeonekana kuwakera wanaharakati wa kutetea haki za kibinadamu.

Kupitia taarifa, Maraga amesema hatua hiyo itaendeleza ukandamizaji wa haki za kibinadamu.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *