#Local News

SERIKALI YAKANA ‘RIPOTI YA KNEC’

Imeibuka kwamba baadhi ya wanafunzi waliopelekwa katika shule za sekondari ya juu bila sare wala karo jinsi ilivyoagizwa na serikali, hawakuendelea na masomo yao baada ya kurejeshwa nyumbani.

Kulingana na wanafunzi hao kutoka mitaa ya mabanda jijini Nairobi, walirejeshwa nyumbani baada ya kupelekwa na maafisa wa serikali, ukiwa ni muda mfupi baada ya baraza la mitihani ya kitaifa KNEC kufichua kuwa zaidi ya wanafunzi 150,000 wa mtihani wa kwanza wa CBE waliachia masomo njiani.

Hata hivyo, wizara ya elimu imeendelea kupinga ripoti hiyo.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *