WAFANYAKAZI WATAKA “COTU’ MBADALA
Kundi la wafanyakazi nchini likiongozwa na aliyekuwa naibu rais Rigathi Gachagua, limependekeza kubuniwa kwa muungano mbadala wa vyama vya wafanyakazi kutoa ushindani kwa ule wa COTU, kwa misingi kwamba COTU imeshindwa kuwawakilisha wafanyakazi ipasavyo.
Miongoni mwa misingi ya kubuniwa kwa muungano huo ni madai kwamba katibu mkuu wa COTU Francis Atwoli, imeshirikiana na serikali ya Rais William Ruto licha ya serikali hiyo kuidhinisha kukatwa kwa makato wanayoyataja kuwa makubwa ya mishahara ya wafanyakazi.
Aidha, wamemtuhumu Atwoli kuwa mbinafasi.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































