#Football #Sports

KOMPANY AAHIDI MCHEZO ‘KUJITOLEA MHANGA’ DHIDI YA PSG

Pambano kali linatarajiwa leo usiku katika mechi ya mkondo wa pili wa semi fainali ya kombe la klabu bingwa bara Ulaya, miamba wa soka nchini Ujerumani Bayern Munchen watakapoialika bingwa mtetezi PSG.

Kocha mkuu wa Bayern Vincent Kompany, ameahidi kuwa kikosi chake kitacheza mchezo wa kushambulia bila kujali tahadhari, jinsi walivyofanya katika mkondo wa kwanza ili kufuzu fainali.

Katika mechi ya mkondo wa kwanza ugani Parc de Princes, wenyeji PSG walipata ushindi wa mabao 5-4, na kuwaweka katika nafasi nzuri ya kufuzu.

Licha ya mechi hiyo kutajwa kuwa bora zaidi katika hitoria ya kombe hilo, Kompany na vijana wake wamekosolewa kwa kuvuja kupindukia katika safu ya ulinzi.

Hata hivyo, beki huyo wa zamani wa kati, amesema hatabadili chochote na badala yake atawatuma wachezaji wake kushambulia katika juhudi za kubatilisha matokeo ya mkondo wa kwanza na kutinga fainali.

Kwa upande wake, kocha mkuu wa PSG Luis Enrique, amesema kwamba vijana wake watahitaji kufunga mabao yasiyopungua matatu ili kufuzu, kauli inayoashiria mchezo wa kushambulia kutoka kwa timu yake. 

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *