Ideal Mobile Online Gambling Enterprises: A Full Guide

With the ever-increasing popularity of on-line casinos, it’s not a surprise that mobile gambling has actually become the following big thing in the sector. Gone are the days when gamers were constrained to their desktops; currently, they can enjoy their favored casino games on the go, anytime and anywhere. In this post, we’ll discover the […]

WASWA AAPA KUIPA AFC LEOPARDS UBINGWA

Mshambuliaji mpya wa AFC Leopards Andrew Waswa amesema analenga kuisaidia klabu hiyo kutwaa mataji msimu huu, akiahidi kutumia tajriba na mafunzo aliyopata nchini Uingereza kuimarisha kikosi cha Ingwe kwenye Ligi Kuu ya Kenya. Akizungumza baada ya kujiunga na klabu hiyo, Waswa amesema mafunzo yake katika chuo cha International House of Manchester yalimpa uzoefu wa kiwango […]

RISING STARLETS YAPANIA HATUA NYINGINE DHIDI YA TANZANIA

Rising Starlets wana matumaini ya kufuzu raundi inayofuata ya kufuzu Kombe la Dunia la FIFA kwa Wanawake chini ya miaka 20 wanapojiandaa kuvaana na Tanzania katika mechi ya marudiano itakayochezwa Jumamosi jijini Dar es Salaam. Kenya inaongoza kwa bao 1-0 kutoka mkondo wa kwanza uliochezwa Februari 7jijini Nairobi. Bao hilo la ushindi lilifungwa dakika za […]

SIFUNA APATA AFUENI YA MAHAKAMA

Katibu Mkuu wa chama cha ODM, Edwin Sifuna, amepata ushindi baada ya Mahakama ya Migogoro ya Vyama vya Kisiasa kusimamisha juhudi za kumfuta wadhifa wake. Mahakama hiyo imezuia utekelezaji wa azimio lililopitishwa na Kamati Kuu ya Kitaifa (NEC) ya ODM, linalolenga kumfukuza Sifuna. Aidha, mahakama imezuia wahusika kutangaza azimio hilo katika Gazeti la Kenya, hatua ambayo […]

ORENGO: SIFUNA BADO NI KATIBU MKUU HALALI WA ODM

Gavana wa Siaya James Orengo amesisitiza kuwa Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna bado ndiye Katibu Mkuu halali wa chama cha ODM. Akizungumza na wanahabari, Orengo amesema kuwa kwa mujibu wa taratibu za chama, Sifuna bado anatambuliwa kisheria kama mshikiliaji wa wadhifa huo, akipuuza hatua zilizochukuliwa na Kamati Kuu ya Kitaifa (NEC) kumwondoa. Orengo amemtetea Sifuna […]

SIFUNA APINGA KUFUTWA UKATIBU MKUU ODM

Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna amepinga uamuzi wa kumwondoa katika wadhifa wa Katibu Mkuu wa chama cha Orange Democratic Movement (ODM), akisisitiza kuwa bado ndiye kiongozi halali aliyechaguliwa kushika nafasi hiyo. Akizungumza katika mkutano na wanahabari jijini Nairobi siku moja baada ya Kamati Kuu ya Kitaifa (NEC) kuamua kumvua majukumu, Sifuna ametaja uamuzi huo kuwa […]

OBURU ASEMA ODM INALENGA KITI CHA NAIBU RAIS

Kinara wa ODM Dkt. Oburu Oginga amesema chama cha chungwa kiko tayari kuanza mazungumzo na chama cha UDA kikilenga kupata nafasi ya Naibu Rais. Kauli hiyo inaashiria mabadiliko ya msimamo wake baada ya hapo awali kumhakikishia Naibu Rais Profesa Kithure Kindiki kuwa ODM haikuwa na nia ya kutwaa kiti chake. Akizungumza katika mkutano na wajumbe […]

KINYANG’ANYIRO CHA EPL CHASHIKA KASI

Manchester City walitia joto kinyang’anyiro cha kuwania ubingwa wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza, EPL, baada ya kupata ushindi kwa ulaini wa mabao 3-30 nyumbani dhidi ya Fulham, na kupunguza pengo la pointi kati yao na viongozi Arsenal. Arsenal, ambao katika misimu 2, 3 iliyopita waliyumba na kupoteza uongozi kutokana na shinikizo la City, […]

ATI ATI ZA KUAHIRISHA CAF 2027

Huenda dimba la mataifa bingwa barani Afrika mwaka ujao AFCON 2027 lililoratibiwa kuandaliwa na Kenya, Tanzania na Uganda likaahirshwa kutokana na ripoti kwamba mataifa hayo hayajajiandaa ipasavyo kuandaa dimba hilo. Iwapo kipute cha mwaka ujao kitaahirishwa, shirikisho la soka barani Afrika CAF litalazimika kufutilia mbali Makala moja ya kipute hicho, linapojiandaa kuanzisha awamu mpya ambako […]

WORLD RUGBY SVNS YASIFIA RAGA YA KENYA

Shirikisho la raga ya wachezaji 7 kila upande ulimwenguni World Rugby Sevens, limeimarisha juhudi zake za kukuza mchezo huo nchini, kwa lengo la kuifanya Kenya kuwa kitovu muhimu cha raga barani Afrika. Shirikisho hilo linaangazia kujenga ushirikiano endelevu na kuongeza idadi ya wanaoshiriki, kukuza vipaji na kuimarisha mchezo wa raga kwa jumla. Msimamizi wa kitengo […]