#Local News

TATIZO LA UHABA WA MAFUTA NCHINI HATIMAYE LATATULIWA

Wahudumu wa magari ya umaa pamoja na wa kibinafsi sasa wana kila sababu ya
kutabasamu baada ya tatizo la uhaba wa mafuta lililoshuhudiwa nchini mapema leo
kutatuliwa huku hali ya kawaida ikiripotiwa kurejea katika vituo vya mafuta mbalimbali
nchini.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari Waziri wa kawi Opiyo Wandayi anasema kuwa
uhaba huo ulisababishwa na hitilafu za kiufundi za kiutawala zilizoathiri usambazaji wa
bidhaa za mafuta katika baadhi ya kampuni nchini na kukana madai kuwa uhaba huo
ulisababishwa na ukosefu wa mafuta nchini.
Juhudi za kuongeza upatikanaji wa mafuta katika maeneo yaliyoathirika tayari zimeanza
huku serikali ikiahidi matumaini ya kurejea kwa hali ya kawaida kufikia leo jioni, Waziri
Wandayi akiwahakikishia wakenya kuwa kuna akiba ya kutosha ya mafuta kukidhi
mahitaji ya sasa akiwataka wananchi kuwa watulivu.

Imetayarishwa na Hilda Ajema

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *