MAJAJI 15 WATEULIWA NA RAIS

Rais William Ruto amewateua rasmi majaji 15 katika mahakama ya rufaa, na kuashiria hatua muhimu katika kuimarisha mfumo wa haki nchini. uteuzi huo ulichapishwa katika toleo maalum la gazeti la Kenya la tarehe 27 januari, 2026, na kusambazwa kwenye x na katibu mkuu wa utumishi wa umma Felix Kosgei. hatua hiyo inafuatia mapendekezo ya tume ya huduma […]

BAYERN KATIKA MAZUNGUMZO YA KUMUONGEZEA KANE MKATABA

Mkurugenzi wa michezo wa Bayern Munich Max Eberl amethibitishakuwa klabu hiyo iko katika mazungumzo ya kumuongezea mkatabamshambuliaji Harry Kane. Kane mwenye umri wa miaka 32 alijiunga na Bayern mwaka 2023 nakwa sasa ana mkataba unaoendelea hadi 2027. Tangu ajiunge naBayern, mshambuliaji huyo wa England amefunga mabao 119 katikamechi 126 na kuchangia pasi za mabao 30. […]

AK YAFUTA MAJARIBIO YA TAIFA YA MASHINDANO YA NDANI

Shirikisho la Riadha Athletics Kenya limefuta majaribio ya kitaifa yakuchagua timu ya Mashindano ya Dunia ya Riadha ya Ndaniyaliyokuwa yamepangwa kufanyika Januari 30–31 jijini Nairobi. Katika taarifa iliyotolewa Jumatatu, AK imesema uamuzi huoumetokana na sababu zisizoepukika. Shirikisho hilo limeeleza kuwa timu itakayoiwakilisha Kenya sasaitachaguliwa kwa kuzingatia viwango vya muda na ubora wawanariadha baada ya dirisha […]

MUNYAO ALENGA MWANZO MKALI TOKYO

Bingwa wa Marathon ya London 2024 Alexander Munyao anaaminikuwa matokeo mazuri katika Marathon ya Tokyo mnamo Machi 1yatakuwa kichocheo cha msimu mkali wa mwaka 2026. Munyao ni miongoni mwa wanariadha wakubwa waliotangazwa nawaandaaji wa mbio hizo kuongoza duru ya kwanza ya msururu waAbbott World Marathon Majors wenye mbio saba. Mbio hizo zitakuwa mara yake ya […]

Inexpensive Therapy Online: A Comprehensive Guide

Treatment is a vital element of mental health care, yet sadly, it can frequently include a hefty price. Nevertheless, thanks to the development of innovation, online therapy has become an extra budget friendly and available alternative for those in requirement. In this write-up, we will certainly explore the world of low-cost treatment online, discovering

KRA: WAKENYA ZAIDI YA 390,000 WASHINDWA KULIPA USHURU WA KSH759B

Mamlaka ya kukusanya ushuru nchini (KRA) imetambua kampuni 392,162 na watu matajiri wanaodaiwa ushuru wa hadi shilingi bilioni 759.7 ambao hawajafanya malipo ya ushuru kwa shirika hilo.Kulingana na ripoti, watu wanaolengwa hivi karibuni wanaweza kukabiliwa na marufuku ya kusafiri, kufungiwa kwa mali, na kuzima Nambari za Utambulisho wa Kibinafsi (PIN). Matokeo hayo yanafuatia ukaguzi wa sajili ya kodi iliyozuiliwa, ambayo […]

LIGI YA MABINGWA ULAYA: USIKU WA MWISHO WA MAAMUZI

Kesho usiku ni siku ya mwisho ya hatua ya ligi ya UEFA Champions League, huku mvutano wa kujikatia tiketi ya moja kwa moja kwenda raundi ya 16 ukifikia kilele. Kwa mfumo mpya, timu nane za juu pekee ndizo zitafuzu moja kwa moja, huku zilizomaliza nafasi ya tisa hadi 24 zikilazimika kupitia mchujo wa play-offs. Baadhi ya […]

STARLETS WAONYWA DHIDI YA KUIDHARAU TANZANIA

Kipa wa kikosi cha Rising Starlets Christine Adhiambo, amewataka wachezaji wenza kuwa makini wanapojiandaa kwa mechi ya raundi ya 3 ya kufuzu dimba la kombe la dunia la wanawake wasiozidi umri wa miaka 20 yaani FIFA U20 Women’s World Cup, akisema mechi hiyo haitakuwa rahisi. Adhiambo ameonya kuwa tofauti na wengi wanavyodhani, kikosi cha Tanzania […]

AFCON 2027: SOKA YA KENYA KUTATIZIKA

Klabu za hapa nchini zitalazimika kusaka viwanja mbadala kwa mechi zao za ligi kutokana na mpango wa serikali kufunga viwanja vikuu vya Nyayo na Kasarani kupisha ukarabati ili kuafikia viwango vya viwanja vya soka vya Morocco kabla ya dimba la AFCON mwaka ujao. Dimba hilo la mataifa bingwa barani Afrika litaandaliwa na mataifa matatu ambayo […]

OTICHILLO ACHUNGUZWA KUHUSU SHEREHE GHALI

Gavana wa Vihiga Wilber Otichillo amejipata kwenye darubini ya maseneta kuhusiana na tuhuma za kutumia shilingi milioni 5 kwa sherehe za kuzindua makazi rasmi ya spika wa bunge la kaunti hiyo, matumizi ambayo mkaguzi wa hesabu za serikali ameyataja kuwa ubadhirifu na haramu. Kamati ya uhasibu wa fedha za kaunti katika bunge la seneti chini […]