MIGORI YOUTH WASALIA KWENYE USAKANI NSL

Migori Youth walidumisha uongozi wao wa ligi ya divisheni ya pili, National Super League, NSL, licha ya sare ya kutofungana dhidi ya Soy United hapo jana. Sare hiyo iliwafikishia pointi 37, sawa na Mombasa United walioandikisha ushindi wa bao 1-0 ugenini dhidi ya Kabatini Youth. Hayo yakijiri, Soy United walidumisha rekodi yao ya kutopoteza mechi […]

GOR MAHIA WATISHIA WAPINZANI WA KICHAPO

Mabingwa wa kihistoria wa ligi kuu ya soka nchini, KPL, Gor Mahia, wametangaza ubabe wao wa soka na dhamira ya kutwaa tena taji hilo kutokana na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Sofapaka ugani Nyayo Jumamosi. Baada ya tahadhari katika dakika za ufunguzi, Gor walichukua udhibiti wa mechi, wakinyakua uongozi kupitia Frank Odhiambo, Sylvester Owino […]

ODM YASISITIZA MGAO WA 50-50

Chama cha ODM kimesisitiza kuwa mazungumzo ya ushirikiano na chama cha UDA kuelekea uchaguzi mkuu ujao yatahusisha kugawana mamlaka sawa, na kwamba hakitakubali kuingia kwenye ushirikiano huo bila makubaliano ya kuwa na hisa sawa. Kulingana na na mwenyekiti wa kitaifa wa chama hicho Gladys Wanga, ODM itaendelea kuimarisha msingi wake kote nchini, ikiwemo kuwawasilisha wagombea […]

UVAMIZI KANISANI: UPINZANI WATISHIA MAANDAMANO

Wakati uo huo, viongozi wa upinzani wametishia kuitisha maandamano ya kitaifa iwapo waliohusika kupanga na kutekeleza mashambulizi dhidi ya aliyekuwa naibu Rais Rigathi Gachagua kwenye kanisa moja kaunti ya Nyeri hawatakamatwa. Viongozi hao akiwemo Gachagua, kinara wa Wiper Kalonzo Musyoka, Eugene Wamalwa wa DAP-K, Martha Karua wa PLP na naibu kinara wa Jubilee Fred Matiang’i, […]

RUTO AAMURU POLISI KULINDA MAKANISA

Rais William Ruto ameviamrisha vikosi vya usalama kuweka usalama wa kutosha kwa makanisa na maeneo yote ya kuabudu, baada ya visa vya ibada kuvurugwa na makundi ya wahuni kuongezeka katika siku za hivi karibuni. Akizungumza jijini Nairobi, Rais Ruto amesema kwamba serikali yake haitaruhusu tena makanisa kuvamiwa na makundi aliyosema yanajitafutia umaarufu wa kisiasa katika […]

OGAMBA AWATAKA WALIMU KASKAZINI KUVUMILIA

Walimu wanaohudumu katika maeneo ya Kaskazini Mashariki mwa Kenya waliotaka kuhamishwa kutokana na utovu wa usalama wametakiwa kuwa watulivu serikali inapoimarisha usalama. Waziri wa Elimu Julius Ogamba, amesema serikali itazingatia maombi ya walimu hao iwapo visa vya utovu wa usalama vitaongezeka, ila akawahakikishia usalama kutoka kwa serikali. Imetayarishwa na Antony Nyongesa

It made a big impression on testers

The 7 Greatest Egg Vibrators In 2022: Amazon, Lovehoney, Good Vibrations I lastly kicked an ex out of my house and scrubbed the place down, removing any remaining ex “residue.” I additionally saged my complete condo and lit a house-blessing candle. Witches understand the significance of cleansing energies as well as mud and skin particles. […]

MATIANG’I APUUZA MADAI YA DUALE KUHUSU CBC

Naibu Kiongozi wa Chama cha Jubilee, Fred Matiang’i, amepuuzilia mbali madai ya Waziri wa Afya Aden Duale kwamba ndiye chanzo cha changamoto zinazokumba Mfumo wa Elimu wa CBC, akisema tatizo haliko kwenye mtaala bali kwenye uongozi wa serikali ya sasa. Katika taarifa aliyotoa kufuatia kauli ya Duale kwenye mahojiano na runinga moja humu nchini, Matiang’i amesema […]

MECHI ZA WIKIENDI ZINATARAJIWA KUSISIMUA EPL

Wikiendi hii, mashabiki wa Ligi Kuu ya Uingereza wanatarajiwa kufurahia mechi zenye mvuto mkubwa, zikianza Jumamosi na Brighton kukutana na Everton, Leeds kucheza dhidi ya Arsenal, na Wolves kukabiliana na Bournemouth  kisha baadaye Kesi ya usiku itakuwa ni kati ya Liverpool na Newcastle wakati Chelsea itakuwa na changamoto ya kukabiliana na West Ham Jumapili, Aston Villa itacheza na Brentford, Manchester United itakuwa mwenyeji wa Fulham, na Nottingham Forest inakabiliana na Crystal Palace kisha Tottenham wakabane koo na Manchester City Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

MATANO AONA MECHI YA KPL KAMA JARIBIO MUHIMU KWA KCB

Kocha wa KCB, Robert Matano, ameona safari ya Jumamosi kwenda Kasarani Annex kama jaribio muhimu kwa timu yake. KCB wapo nafasi ya tisa katika jedwali la SportPesa League wakiwa na alama 25 kutokana na michezo 18, baada ya kupoteza kwa mabao 2-1 dhidi ya Tusker, jambo lililoacha wachezaji na ufundi wakitamani kuonyesha uwezo wa kujirekebisha haraka. Mechi hiyo […]