ORENGO: ODM KUBWA KWA UDA, DEBENI TUPO
Viongozi wa ODM wanaoegemea mrengo wa Linda Mwananchi wamesisitiza kuwa ni sharti chama hicho kiwe na mgombeaji wa urais kwenye uchaguzi mkuu ujao, kwa misingi kwamba ODM ndicho chama kikubwa kiliochosalia nchini.
Kwenye mahojiano na shirika moja la habari, gavana wa Siaya James Orengo, amedai kuwa mrengo wa seneta wa Siaya Oburu Oginga umekuwa ukifanya baadhi ya maamuzi kwa maelekezo ya Rais William Ruto, akikariri kauli yake kwamba ndiye kaimu kinara wa chama hicho.
Amewatuhumu manaibu kinara wa chama hicho na mwenyekiti wa kitaifa, kwa madai ya kukiyumbisha chama hicho.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 














































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































