UCHUNGUZI WA DCI KUHUSU KIFO CHA JIRONGO

Aliyekuwa mbunge wa Lugari Cyrus Jirongo alifariki kwenye ajali ya kawaida na wala hakuna uhalifu uliohusika kutokana na ushahidi uliopo. Haya ni kulingana na taarifa ya idara ya upelelezi DCI, ambayo imeripoti kuwahoji na kuandikisha taarifa kutoka kwa watu kadhaa akiwemo spika wa bunge la kitaifa Moses Wetang’ula, dereva wa basi la Climax Coaches Tiras […]

WAZAZI NJIA PANDA KUHUSU GRADE 10

Baadhi ya wazazi wamejipata katika hali ya mkanganyiko kuhusu hatma ya masomo ya wanao wanaofaa kujiunga na gredi ya 10 wiki ijayo, baada ya kukumbwa na dosari katika mchakato wa kuwaweka katika shule za kujiunga nazo. Wakizungumza na wanahabari, wazazi waliokosa kurudhishwa na shule walizowekwa wanao wamelalamikia madai ya serikali kutojali, wakiitaka kuangazia upya mchakato […]

ALAI AKANA KUMSHAMBULIA BABU

Mwakilishi wa wadi ya Kileleshwa jijini Nairobi Robert Alai, amekana madai ya kumshambulia mbunge wa Embakasi East Babu Owino mtaani Kilimani. Kwenye mazungumzo na kituo kimoja cha runinga mapema leo, Alai amekiri kuwepo kwa majibizano baina yao kuhusu wadhifa wa ugavana kwenye uchaguzi mkuu ujao ila akakana kumshambulia. Wawili hao wanachunguzwa na polisi kuhusu madai […]

LUSAKA AHIMIZA UADILIFU SERIKALINI MWAKE

Maafisa wa serikali ya kaunti ya Bungoma wametakiwa kudumisha uadilifu, umoja na uwajibikaji serikali hiyo inapoangazia kuimarisha utendakazi na ukamilishaji wa miradi ya maendeleo iliyokwama. Akizungumza mapema leo kwenye kikao na wafanyakazi hao, gavana wa Bungoma Ken Lusaka amesema hatua hiyo ni muhimu katika utendakazi wa serikali hiyo kwa wananchi. Kulingana na naye, migawanyiko itakwamisha […]

JESHI LA VENEZUELA LAMTAMBUA KIONGOZI MPYA

Jeshi la Venezuela limetangaza kumuunga mkono aliyekuwa makamu wa Rais Nicolas Maduro aliyebanduliwa na Marekani, Delcy Rodriguez kuwa rais wa taifa hilo baada ya kuapishwa. Waziri wa ulinzi nchini humo Vladimir Padrino Lopez ameashiria kumuunga mkono Rodriguez ambaye rais wa Marekani Donald Trump amesema ni kiongozi mwafaka ambaye Marekani inaweza kufanya naye kazi. Kupitia hotuba […]

10 WAFARIKI KWENYE AJALI NAIVASHA

Idadi ya waliofariki kwenye ajali ya barabara karibu na Karai eneo la Naivasha usiku wa kuamkia leo imepanda hadi 10 huku watu wengine 5 wakiwa katika hali mahututi. Ajali hiyo imehusisha basi la kampuni ya Greenline lililokuwa likielekea Nairobi na matatu iliyokuwa ikielekea Nakuru, polisi wakisema 8 kati ya waathiriwa walikuwa abiria wa matatu na […]

DIVISHENI ZA KEIYO, KAPOMBOI KUANZA HUDUMA

Serikali imepania kurahisisha upatikanaji wa huduma zake muhimu kwa wananchi katika kaunti ya Trans Nzoia kupitia kuanzishwa kwa divisheni 2 za Keiyo na Kapomboi na kata ndogo ya Teitei katika eneo bunge la Kwanza kaunti hiyo. Tangazo hilo limewekwa wazi na Waziri wa usalama wa kitaifa Kipchumba Murkomen ambaye pia amesema serikali ina mpango wa […]

CITY WAONYESHWA VIMULIMULI VYA BLUES

Bao la Enzo Fernandez dakika za mwisho ziliipa Chelsea pointi 1 muhimu kwenye sare ya bao 1 na Manchester City na kudidimiza matumaini ya City kushindana na Arsenal katika uwandaji wa taji la ligi kuu ya soka nchini Uingereza EPL. Kiungo wa Uholanzi Tijjan Reijnders aliwaweka City kifua mbele kabla ya kipindi cha kwanza kutamatika […]

CAMEROON WAKATA TIKETI DHIDI YA MOROCCO

Timu ya taifa ya Cameroon itamenyana na wenyeji wa dimba la taifa bingwa barani Afrika AFCON Morocco kwenye robo fainali ya dimba hilo, baada ya kuwalaza Afrika Kusini mabao 2-1 kwenye pambano lililojaa mihemko. Baada ya kuanza kwa kishindo, Afrika Kusini waligutushwa na bao la beki wa Stoke City Junior Tchamadeu katika dakika ya 34 […]