WAKENYA WAPEWA NAFASI KUBWA MARATHON YA COPENHAGEN
Wanariadha wa Kenya wanatarajiwa kuwa miongoni mwa washindani wakuu katika toleo la 46 la Copenhagen Marathon litakalofanyika Jumapili nchini Denmark.
Vincent Mutai anaongoza orodha ya wanariadha wa wanaume baada ya kumaliza wa pili mwaka uliopita, ambapo aliweka rekodi yake bora ya saa 2:09:09 katika mbio hizo za mji wa Copenhagen.
Mutai ni sehemu ya kikosi imara cha wanariadha wa kimataifa, huku mwanariadha wa Ubelgiji Lahsene Bouchikhi akiwa Mzungu pekee miongoni mwa washindani wakuu waliowahi kukimbia chini ya saa 2 na dakika 10.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































