SERIKALI YAFICHUA WAKENYA WALIOUAWA URUSI
Imeripotiwa kuwa wakenya wasiopungua 19 wameuawa katika mapigano yanayoendelea kati ya Urusi na Ukraine, serikali ikisema wakenya 291 wamethibitishwa kuajiriwa kama wanajeshi wa Urusi.
Akiwa mbele ya kamati ya uajiri na Leba katika bunge la seneti, Waziri wa masuala ya kigeni Musalia Mudavadi, amesema wakenya 42 hawajulikani waliko huku wengine 2 wakizuiliwa kama wafungwa wa kivita nchini Ukraine.
Amesema serikali inaendeleza juhudi za kuwarejesha nchini.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 




































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































