EUROPA: VILLA, FREIBURG KUMENYANA FAINALI, PALACE FAINALI CONF.
Klabu ya Aston Villa imesalia na mechi moja pekee kabla ya kutamatisha ukame wa kupata taji kuu kwa kipindi cha miaka 30, baada ya kutua fainali za kombe la UROPA League jana usiku kufuatia ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Nottingham Forest.
John McGinn alifunga mara mbili na kuongeza kwa bao la Emi Buendia la mkwaju wa penalty kunako dakika ya 53 na bao la ufunguzi na Ollie Watkins mwishoni mwa kipindi cha kwanza, na kuipa Villa ushindi wa jumla ya mabao 4-1.
Kutokana na ushindi huo, Villa watamenyana Freiburg ya Ujerumani kwenye fainali ya ligi hiyo tarehe 20 mwezi huu jijini Istanbul nchini Uturuki, kocha mkuu Unai Emery akilenga kushinda ligi hiyo kwa mara ya 5 baada ya kushinda mara 3 akiwa na Sevilla na mara 1 akiwa na Villareal nchini Uhispania.
Freiburg kwa upande wao walitinga fainali hizo baada ya kuwalaza kwa mabao 3-1, na jumla ya mabao 4-3.
Villa wanashikilia nafasi ya 5 katika ligi kuu ya Uingereza, EPL, na iwapo watashinda taji la UROPA, timu iliyo katika nafasi ya 6, ambayo ni AFC Bournemouth kwa sasa, itapata fursa ya kushiriki ligi ya mabingwa bara Ulaya mwishoni ujao.
Katika fainali ya Conference League, Crystal Palace ya Uingereza itamenyana na Rayo Vallecano ya Uhispania tarehe 27 mwezi huu katika uwanja wa Red Bull Arena jijini Leipzig nchini Ujerumani.
Palace waliilaza Shaktar Donetsk jumla ya mabao 5-2 huku Freiburg wakiilaza Strasbourg jumla ya mabao 2-0 katika awamu ya semi fainali jana usiku.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 




































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































